Willy Paul amtafutia kazi Mcee mkubwa nchini

25036537_156940708364886_7868735838413127680_n__1561100948_46217
25036537_156940708364886_7868735838413127680_n__1561100948_46217
Mtaalam na nguli wa muziki Willy Paul amempa shavu kubwa Mcee aliyemsaidia kutoka kisanaa nchini . Huku akionyesha tabasamu kubwa, Mcee huyu amefunguka mwanzo mwisho jinsi staa wa muziki wa injili Willy Paul alimpiga mpunga wa laki 4 za kwake ili kusherehesha katika tamasha la burudani.

Katika posti refu zaidi katika mtandao wake maridhawa wa instagram, staa huyu alichapisha ujumbe unaonyesha jinsi Pozze alimpa kazi ya kusherehesha katika tamasha zake 29 zilizoratibiwa kufanyika nchi tofauti.

Ikumbukwe kwamba Mcee huyu ndiye alisaidia kuipaisha juu nyota ya muziki ya Willy Pozze miaka michache iliyopita. Willy kumpa kibarua cha kusherehesha katika fiesta zake ni mfano mzuri wa kufaana katika tasnia hii ya burudani.

Soma hapa:

Mcee huyo amefunguka jinsi staa huyu anayetamba freshi na kibao cha Halleluyah alimpigia simu na kuomba wakutane katika hoteli ya Sankara na kumpiga pesa lukuki mfukoni elfu 400,000.

Baada ya mcee huyo kumkubalia ombi la kufanya kazi pamoja, Pozze alijawa na furaha zaidi.

Soma hadithi nyingine:

"Tupige kazi tuonyeshe ulimwengu kuwa Kenya imejaliwa sana. Tufanye kazi pamoja. Nashukuru umekubali tupige kazi." Alisema Willy Paul.

Soma hapa:

Msanii huyu ana ratiba kubwa ya misururu ya tamasha 29 katika nchi mbalimbali ikiwemo Amerika Kusini, Nigeria, Tanzania na kibao Kenya.