Willy-paul-696x522

Willy Paul anataka mwanamke, sio mke

Willy Paul ameweka wazi kwamba anataka mwanamke ambaye atakuwa mwandani wake ila hatamuoa. Amesema anawezakuwa katika mahusiano zaidi ya miaka thelathini bila kuoa.

“Kwanini nioe? Nataka mwanamke lakini sio mke” Mwanamziki huyo aliongea katika njia ya simu na ripota wetu.

Aliendelea kusema kwamba yeye hayuko katika Uhusiano ijapokua anaimba nyimbo ambazo ni za mapenzi.

“Siko kwenye uhusiano wowote, wanawake ni watu wagumu sana. Nimejifunza kwa maisha na siyaamini mapenzi”

Willy Paul
Willy Paul

Hata hivyo, Mali Queen, ambaye ni mzazi mwenza wa Willy Paul,aliambia wasichana wakae mbali na mumewe.

“Wasichana, Willy Paul amechukuliwa na hivi karibuni tutafunga ndoa. Mimi ni mama wa mtoto wake #KingDamian..Wasichana kaeni mbali, msimletee majaribu.”

Lakini je! Willy Paul na Mali Queen wako katika mahusiano?

willypaulnewlook

Willy Paul amtafutia kazi Mcee mkubwa nchini

 

Photo Credits: Instagram

Read More:

Comments

comments