Willy Paul ateta masaibu yake na Rayvanny. Afunguka uovu wote

Staa na muimbaji tata Willy Paul sasa anampa dongo staa wa WCB Rayvanny kwa kile anachokitaja kama wizi wa ngoma ya Chuchuma.

Kulingana na Pozze, ubunifu wa mkwaju wa Chuchuma ulikuwa wa kwake kutoka mwanzoni.

Baada ya kudondosha mkwaju huu juma lililopita, Willy Paul aliwashangaza mashabiki kwa vijimaneno alivyochapisha katika mitandao ya kijamii.

Soma hadithi nyingine:

Katika vijimaneno hivi staa huyu anaonekana kumlenga Rayvanny. Ikumbukwe kuwa Rayvanny alikuwa ameangusha ngoma yenye mdundo sawa na Willy Paul.

Inaonekana kuwa ngoma hii walitakiwa waifanye pamoja ila kukawa na kutoelewana. Rayvanny amemshirikisha nyota wa kike Nora Fatehi.

Collabo ya Rayvanny na Fatehi inafanya vizuri katika mtandao wa You Tube ikilinganishwa na yake Willy Paul.

"Alibadilisha kila kitu katika ile nyimbo. Nikakataa. Halafu nikawa nafikiria hilo ni tatizo ndogo ambalo hatufai kuwa nalo. Sisi ni mandugu, urafiki wetu unafaa kwa wa kwanza. Tuendelee kuwa marafiki ila nitafanya nyimbo yangu kwa sababu naipenda jinsi ilivyo." Alisema Pozze.

Baada ya uamuzi huu Pozze anasema kuwa Rayvanny alimfungia mawasiliano katika simu.

"Nikashangaa sana. Ishakua sasa tunachukiana wenyewe."

Soma hadithi nyingine:

 Baada ya siku chache, Willy Paul anasema kuwa alishangaa kuona mdundo huo ukipepea katika mitandao ya insta ya RayVanny.

"Vesi yake katika ngoma na Fatehi imetokana na utunzi wa rekodi za sauti nilizomtumia. Sio vizuri."

Hii sio mara ya kwanza Willy Paul kuwa katika matatizo na nyota wa bongo. Mwaka uliopita, alifanya ngoma na Konde Boy na baadaye kukosana.

Harmonize alitoa hiyo ngoma na akaipa shavu kubwa zaidi kupita collabo yake na Pozze.