Wito wa Afrika! Bara la Afrika ni sharti lijumuishwe katika mikakati inayoendelea ya kubaini jinsi ya kukomesha corona

Viongozi wa mataifa ya Afrika wamesema ni sharti mataifa ya Kiafrika yahusishwe katika mchakato unaoendelea wa kutafuta suluhisho la kudumu katika janga ambalo limeathiri ulimwengu mzima la Corona.

Viongozi hao wakiwemo Uhurun Kenyatta wa Kenya, Macky Sally wa Senegal, Allasane Outtara wa Ivory Coast, Julius aada Bio wa Sierra Leone na Mahamadou Issoufou wa Nigeria wamesema hayo katika mkutano uliofanyika kwa njia ya video na uliongozwa na shirika la New York Forum Institute.

Akizungumza katika mkutano huo, kiongozi wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema ni sharti mataifa mengine ulimwenguni kuona bara la Afrika kama mataifa mengine yanayoendelea kutafuta suluhisho la kudumu kutokana na virusi hivyo hatari.

“Africa is not the problem but through partnership we can be a solution.”  President Kenyatta told the pan-African panel. Amesema Kenyatta

Amesema wakati huu ambapo mataifa mengi yameathirika na virusi hivyo hatari, ni sharti mataifa kuungana na kuwa kitu kimoja ili kupata suluhu la kudumu.

“It is quite clear to me and many of my colleagues on the African continent that our success in defeating this particular disease is going to be based both on our individual country response and more importantly on our collective response as a continent,” aliongezea Kenyatta.

Aliongezea kuwa kama Kenya, wamebuni kliniki tamba ambazo zimeweza kuwapima wakenya wengi na kuongeza kuwa asilimia kubwa ya wakenya sasa wameanza kulipia gharama zao za nyumbani kupitia kwa njia ya simu kama njia ya kupunguza maambukizi zaidi.

“In Kenya, technology has played a huge role in the way Kenyans have transacted with each other in the last ten years. Technology has not only provided job opportunities but contributed to the growth of the economy,” amesema Kenyatta.

Amesifia uongozi wa Jumuiya ya Afrika chini ya kiongozi Cyril Ramaphosa kama mwenyekiti, Kenyatta amesema kufikia sasa viongiozi wamekuwa wakishirikiana ili kujadili mbinu mwafaka ya kuzuia maambukizi ya virusi hivyo.

Kwa upande wake rais wa Senegal Sally, amesema virusi vya corona sasa vitayafanya mataifa ya Afrika kufikiria haswa kuhusiana na jinsi ya kuekeza na kutenga pesa nyingi kwa matukio ya majanga kama haya.

Ameyataka mashirika ya kimataifa kujumuisha mataifa ya Afrika katika jitihada zake.

Maoni ambayo yaliungwa mkono na viongozi wengine Allasane Outtara, Julius Maada Bio na Mahamadou.