Wizara ya afya inapanga kuwaajiri zaidi ya wahudumu 4000 wa matibabu

Wizara ya afya inalpanga kuwajiri zaidi ya wahudumu 4000 wa matibabu walio katika mafunzo ili kutoa usaidizi katika vituo vya afya vya umma.

Serikali pia inalenga kuwaajiri watalaam 250 wa afya ili kusaidia katika utekelezaji wa mpango wa kutoa huduma za afya kwa wote bila malipo.

Mkusanyiko wa habari

Gavana wa kakamega jana aliwaongoza wakaazi kwa siku ya pili ya kuusafisha mji huo na kubomoa vibanda kando ya barabara. Oparanya amesema hana imani tena na wafanyikazi wa kaunti hiyo .

Seneta wa busia Amos Wako ameupuuzilia mbali mkutano wa viongozi wa jamii ya waluhya unaoandaliwa na katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli. Amesema mkutano huo unalenga kuwanufaisha watu binafsi kisiasa kwani sio viongozi wote walioalikwa.

Wizara ya elimu imesema kwamba mwongozo wa karo za shule uliotumiwa mwaka jana ndio unaofaa kutumiwa mwaka huua. Wizara hiyo  imesema haijawashauri walimu wakuu kuongeza karo za shule na shule zitakazofanya hivyo zinafaa kuripotiwa mara moja.

Wanaume zaidi kuliko wanawake wanajiua kwa sababua wanawake hupata usaidizi haraka ili kushughulikia matatizo yaoa. Mwanasaikolojia Silas Kiriinya  anasema wanaume kwa upande wao huumia kwa sababu jamii imewakuuza na dhana kwamba kuzungumzia matatizo yako ni ishara ya udhaifu.

Rais Donald Trump wa marekani amesema Amerika ilimwua jenerali Qasem Soleimani wa iran ili kuzuia vita na sio kuanzisha mapigano katika eneo la mashariki ya kati. Amesema tishio la mashambulizi la kigaidi yalioongozwa na Soleimani sasa halipo kufuatia kifo chake alipotua katika uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iarq hapo jana.