Wizara ya elimu kufanya uchunguzi katika shule ya upili ya Kangaru

Wizara ya elimu nchini inafanya uchunguzi katika shule ya upili ya Kangaru kufuatia mauaji ya mwanafunzi wa kidato cha tatu baada ya kudaiwa kuchapwa na mwalimu wake hesabati.

Akithibitisha kisa hicho mwelekezi wa elimu wa kaunti ya Kiambu James Kairu alisema kuwa mwanafunzi huyo alifariki akiwa hospitali baada ya kuchapwa na mwalimu wa hesabati.

Kairu alisema kuwa uchunguzi unaendelea na hatua ya dharura itachukuliwa kwa yule atapatikana na hatia ya mauaji hayo.

"Timu ya wataalamu inaendelea kuchunguza kisa hicho, na tutaweza kuchukua hatua kulingana na ripoti yao." Alieleza Kairu kwa njia ya simu.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Kiminda Wambugu alisema kuwa kisa hicho kimeongezwa chumvi na kushindwa kuchunguza zaidi.

"Kisa hicho kimetiwa chumvi, na kama madai hayo ni ya ukweli shule hii haingekuwa na wanafunzi." Alisema Kiminda.

Mwanafunzi aliweza kukata roho akiwa katika hospitali ya Nairobi (Nairobi Women hospital).

Ripoti zilionyesha kuwa mwanafunzi huyo aliweza kuvunja mguu wake akiwa anachapwa na mwalimu huyo, si adhabu tu ya kawaida bali mwalimu huyo alitumia mti wa kupiga deki.

Aliweza kupelekwa na shule hiyo katika hospitali moja ambapo aliweza kufungwa mahali alikuwa ameumia, ni visa tofauti ambavyo vimeweza kutokea katika shule tofauti.

Sababu za mwalimu huyo kumchapa mwanafunzi huyo hakijabainika, ni maswali ambayo wazazi na walimu pia wachunguzi wameweza kubaki nayo kwanini mwalimu kumchapa mwanafunzi huyo hadi kumuumiza.

Baadaye mwanafunzi huyo alipata matatizo na kupelekwa katika kituo kingine cha afya na kulegezwa bendeji aliokuwa amefungwa katika mguu wake.

Baada ya siku kadhaa aliweza kurudishwa katika hospitali ya kwanza na kisha kumuambia aweze kuenda katika hospitali ya wanawake ya Nairobi.

Nguvu za kumfikia mwelekezi wa TSC wa kaunti ziliambulia patupu, hii ni kwasababu hakuweza kupokea simu wala kujibu jumbe ili aweze kupeana maoni yake kuhusu kisa hicho.

Swali kuu ni nani kati ya mwalimu na mwanafunzi huyo alikuwa katika makosa.