Wizara ya michezo yajitetea baada ya wachezaji kufurushwa hotelini

wizara ya michezo
wizara ya michezo
Wizara ya michezo imejitete dhidi ya madai ya kusababisha aibu ya kufurushwa kwa wanamichezo kutoka kwa hoteli yao. Waziri Amina Mohammed anasema kamati za mipango na usimamizi zinazojumuisha maafisa, wawakilishi na wadau ndio walikuwa na jukumu la kupanga na kuratibu kushiriki kwa Kenya kwenye michezo ya All Africa nchini Morocco.

Waziri huyo pia amefichua kuwa bajeti ya shilingi milioni 335 ilikuwa ikidhi mahitaji yao yote ikiwemo malazi wakiwa nchini, marupurupu yao, tikiti za ndege na malazi wakiwa nchini humo.

Timu ya raga ya wachezaji 7 haijaanza mazoezi licha ya KRU kutangaza kuwa wataanza wiki hii. Hata hivyo kocha mpya Kelvin Wambua tayari amekitaja kikosi cha wachezaji 38 na walikuwa wafanyiwe uchunguzi wa kabla ya kuingia kambini jumatatu.

Wanajumuisha baadhi ya wachezaji ambao walisusia kuichezea timu hiyo msimu uliopita na haijabainika iwapo watacheza ikizingatiwa kua KRU bado haijapata mfadhili.

Wambua ambaye amechuku wadhfa huo kutoka kwa Paul Murunga watakipunguza kikosi hicho hadi wachezaji 20 wanaposubiri michuano ya kufuzu wa Olimpiki ya Africa, Novemba nchini Afrika Kusini.

Hayo yakijiri, nahodha wa timu ya raga kinadada nchini Philadelphia Olando anasema watapambana ili kuinyuka Afrika Kusini na kufuzu kwa kombe la dunia la wachezaji 15 kila upande.

Lioneses walilaza majirani Uganda 37-5, katika michuano ya Kombe la ubingwa bara Afrika kwa akinadada. Afrika kusini pia waliwabwaga Uganda na Madagascar na watakua wanawania ushindi ili kujinyakulia tikiti hio.

Kwingineko, mchezaji soka Emiliano Sala alikua na viwango vikubwa vya hewa ya carbon monoxide mwilini kabla ya ajali ya ndege iliyopelekea kifo chake kutokea, ripoti moja imefichua. Sala na rubani David Ibbotson walianguka na ndege tarehe 21 Januari walipokuwa wakielekea Cardiff kutoka Nantes Ufaransa.

Uchunguzi umebaini kuwa mwili wa Sala ulikuwa na viwango vya juu vya hewa hio kwenye damu yake ambavyo hata vilikuwa na uwezo wa  kupoteza fahamu au hata mshtuko wa moyo. Wakili wa familia ya sala anasema ripoti hio inazua maswali zaidi.