sad man

Wololo!Jamaa atoroka kwake baada ya kupewa presha na ‘dem’ yake amuoe

Wakati huu wa janga hili wengi wataona mambo na hata kutenda mambo ambayo hayastahili kwa sababu ya tamaa. Jamaa mmoja kutoka eneo la Athi River amewaacha wengi vinywa wazi na hata kuwashangaza wengi baada ya kufichua kuwa alitoroka kwake kwa ajili ya mpenziwe.

Semasema za mtaani zinaarifu kwamba wawili hao walikuwa wamechumbiana kwa miezi mitatu na uhusiano wao ulikuwa umejulikana na wengi eneo hilo.

Kulingana na nduru za habari, kipusa huyo amekuwa akimtembelea mpenzi wake na kumuarifu aharakishe ili woane.

Mienendo ya demu ilimuudhi jamaa ambaye alihitaji muda zaidi wa kuchumbiana na kujuana lakini kipusa alikuwa na mbio za kutaka kuolewa.

Hata hivyo, siku ya kisanga mrembo alimtembelea lofa kama ilivyokuwa desturi yake asijue yaliyokuwa yanamsubiri.

“Kila siku ukija hapa ni kuniambia nikuoe. Mbona hutaki kunipa muda zaidi nijipange? Mimi siko tayari kuwa na familia kwa sasa.” Alimueleza.

Duru zinasema demu alipoondoka jamaa alifunganya virago na  kuondoka eneo hilo. Baadaye iliibuka kwamba lofa alihamia kwa rafiki yake kwa muda kuhepa shinikizo la demu huyo.

 

Photo Credits: radiojambo

Read More:

Comments

comments