‘Work from home’: Unachofaa kujua kuhusu kufanyia kazi nyumbani  wakati huu wa Coronavirus

fanya kazi
fanya kazi
Baada ya mkurupuko wa virusi vya corona katika sehemu nyingi kote duniani ,kampuni na mashirika mengi yamewataka wafanyikazi wao kufanyia kazi nyumbani ili kuzuia utangamano wa watu wengi afisini na pia wanaposafiri kwenda na kutoka kazini .

Kwa wengi nchini Kenya ,huenda ni mtindo wa kigeni kufanyia kazi nyumbani lakini mwongozo huu unafaa kukupa taswira ya jinsi ya kupambana na hali yako mpya . Haifai kusisitizwa lakini hakikisha umeoga. Usicheke kwa sababu kuna wanaofikiria kwamba wapo nyumbani na hivyo basi hawahitaji kuwa wasafi . Kufanyia kazi nyumbani ni kibarua kikubwa kwa sababu kuna vingi vinavyoweza  kukusumbua fikra na kukupotezea muda muhimu sana.Hali inaweza kuwa ngumu zaidi iwapo nyumbani kuna watoto au watu wengine ambao labda hawana pa kwenda. Kwa sababu umepewa fursa ya kufanyia kazi nyumbani usiichukulie fursa hiyo kama vacation-Kazi lazima iendelee kwa sababu mchango wako unategemewa kuhakikisha kampuni au shirika lako linaendeleza oparesheni au shughuli zake

 Piga mswaki ,valia nguo zako za kawaida

Fahamu kwamba upo kazi.kwa hivyo unafaa kuvalia nadhifu.wakati mwingine utahitajika katika simu ya video na unaonekana katika upande wa pili .Hutaki kuonekana ukiwa bado umevalia  nguo za kulala .Unafaa kuonekana ni kana kwamba upo kazini

 Chukua mapumziko  kama tu unavyofanya afisini

Ukiwa afisini labda wewe huchukua muda wa dakika 15 hivi kwa matembezi ya kunyoosha viungo.basi ukiwa nyumbani ,fanya mazoezi mepesi ili kujichangamsha kabla ya kuenelea na kazi .Kumbuka kuketi mfululizo bila kitu cha kushtukiza mwili pia ni hatua itakayokulegeza akili na hata kukufanya ujipe usingizi usipochunga .

 Wasiliana na msimazi/Mkuu wako mara kwa mara

Jiulize unahitaji nini kutoka kwa mkuu wako naye anahitaji nini kutoka kwako .Kwa sababu mpo mbali na kila mmoja sio kisingizio za kuiweka simu kwenye ‘flight mode’. Ingawaje kuna wasimamizi wenye taasubi za kutaka ukuu ,ambao watakusumbua kila wakati kujua unafanya nini ,hakikisha una mpangilio wa kazi yako na unachofanya kinaonekana katika mifumo inayohitajika . Mawasiliano ya simu ,video na jumbe au hata  kuunda makundi ya ushirikiano ya whatsapp  ni muhimu sana wakati huu ambapo kila mtu yupo mbali. Unafaa kuhakikisha kwamba unafahamu wanachofanya wenzako kokote waliko ili msijipate wote mnafanya kitu kimoja au mmtelekeza kufanya kitu kinachofaa kushughulikiwa .Kama msimamizi ,hakikisha kundi lako zima lina yote yanayohitajika kwa wakati .

 Agiza chakula cha mchna iwapo utakihitji

Iwapo utahitaji kuagiza chakula basi fanya hivyo .Maambukizi ya virusi kupitia kwa  chakula ni jambo adimu sana kulingana na wataalam. Ingawaje unashauriwa kunawa mikono ifaavyo. inashauriwa kutumia angalau sekunde 20 katika kunawa mikono  hasa unapotangamana na mtu anayeleta chakula ulichoagiza . Iwapo ulifanya matayarisho ya kutosha siku yako inaweza kuanza wakati umeshatayarisha utakachokula wakati wa mchana kama tu unavyotayarisha chakula cha mchana ambacho wewe hubeba ukienda kazini

 Wape shughuli wanao

Iwapo wewe ni mzazi wa watoto ambao hawapo shuleni ,itakuwa kazi ngumu kuwaeleza kwamba unahitaji muda wa kufanya kazi na watataka mchezo wa hapa na pale au uwape muda wako . usiogope kuwatafutia michezo ya kuelimisha ya video ili kuwashughulisha kivyao ili upate muda wa kufanya kazi . mchezo wa Minecraft,  kwa mfano ni bora sana kujenga utangamano kati yao na pia kuzua ubunifu katika fikra zao .  Hakuna kigumu  kama kuwathibiti wanao nyumbani .Kwa mfano wanangu wawili Nas  na JJ hawajakubali kwamba sio muda wangu kucheza nao.Tafuta udhaifu wao kuhusu kinachowanata fikra ili ujipe uhuru wa kufanya kazi .

 Tafuta uwiano kati ya kazi na maisha yako

Baada ya kazi usijibane katika mazingira ya afisini .Semezana na rafiki na jamaa zako kwenye simu au video  hasa baada ya muda mrefu wa kujitenga. Pia  haidhuru kuteremsha kitu kikali cha kuwavua misuli kwenye glasi baada ya siku nzima ya kuketi kwenye kompyuta.