Wycliffe Oparanya ataja vigezo BBI inafaa kutimiza ili magavana waunge mkono mapendekezo

pic
pic
Kamati kuu ya magavana ikiongozwa na Oparanya inatarajiwa kufanya kikao na wawakilishi wodi katika harakati za kubaini kuwa wataunga mkono mapendekezo ya BBI ya Uhuru Kenyatta na Raila Odinga au watasalia kupiga hatua katika azma yao kuu ya ya kupigania mgao mkubwa wa pesa katika serikali za kaunti.

Pata uhondo hapa:

Mwenyekiti wa kamati kuu ya magavana Wycliffe Oparanya jana alisema kuwa huduma katika serikali za kaunti huenda zikalemazwa kufuatia hali ya sintofahamu kati ya bunge la kitaifa na seneti.

Pata uhondo hapa:

"Tunatoa mwito wa kupiga kura tubadilishe katiba kwa sababu tunataka mgao mkubwa wa rasilimali uje katika serikali za kaunti. Kwa sasa lengo letu ni kuona kwamba ugatuzi umepata nguvu zaidi ili mwananchi wa kawaida anufaike kwa huduma anazopata." Wycliffe Oparanya

Mwenyekiti wa magavana aidha aliongeza kauli kuwa magavana wataamua iwapo wataunga mkono BBI . Hii itategemea iwapo mapendekezo yanayosubiriwa ya BBI yataangazia ugatuzi kwa mapana na marefu.