Xhaka ashushwa ngazi: Ma staa wengine kuwahi jipata katika hali hii

Hapo jana meneja wa timu ya wanabunduki, almaarufu Arsenal, Unai Emery alitangaza hadharani kuwa klabu hiyo imefikia uamuzi wa kumshusha ngazi, Granit Xhaka kama nahodha.

Uamuzi huu unajia wiki kadhaa baada ya mswidi huyo kukorofishana na kuwazomea mashabiki wa Arsenal kabla ya kuvua jezi na kuondoka ugani Emirates, wakti wa mechi yao dhidi ya Crystal Palace.

Xhaka ambaye hajakuwa akionesha mchezo bora msimu huu na mashabiki hawajapendezwa na hilo na huwa wakimzomea hata kupitia mitandao ya kijamii.

Siku hiyo alipokuwa akitolewa uwanjani, Arsenal ilikuwa imekabana koo na Palace wakiwa sare ya mabao 2-2 na badala ya kuharakisha kutoka uwanjani alitembea tu, na kuwakera mashabiki zaidi ya elfu sitini.

Hapo ndipo alipoamua kuwazomea mashabiki huku akiwaonesha kuwa hakujalishwa nao na wengi walikwazwa huku wakiomba klabu hiyo imshushe ngazi na ikiwezekana auzwe.

Katika kikao na wanahabari kabla ya mechi yao ya ligi ya Europa, Unai alitangaza uamuzi huo huku mshambulizi matata, Pierre-Emerick Aubameyang akipandishwa kutoka naibu nahodha hadi kuwa nahodha.

Aubameyang ataisidiwa na wachezaji wanne wakiwemo; Alex Lacazette, Hector Bellerin na kiungo Mesut Ozil.

Kufuatia hilo, tunaangizia orodha ya wachezaji wengine ambao washawahi jipata katika hali ile ya kushushwa ngazi hapo awali.

  1. William Gallas (Arsenal)

Mwaka wa 2008, mfaransa Gallas alijipata taabani na kocha wake, Arsene Wenger baada ya kuwazomea wachezaji wachanga wa klabu hiyo.

Baadaye, alishushwa ngazi, akakosa mechi kadhaa kabla ya kurushwa nje ya timu hiyo na kujiunga na Tottenham.

2. Branislav Ivanovic (Serbia)

Kama kuna wachezaji bora ambao wamewahi shuhudiwa katika ligi kuu ya Premia ni defender huyu wa kushoto ambaye alicheza na kushinda mataji mengi na Chelsea.

Ivanovic alikuwa nahodha wa nchi yake Serbia tangia 2012 lakini alipoteza wadhfa wake mwaka wa 2018, kabla tu ya dimba la kombe la dunia.

3. Mauro Icardi (Inter Milan)

Msimu uliopita, Icardi alijipata katika vyombo vya habari wakti mazungumzo yake na klabu yake, Inter Milan kuhusu mkataba mpya ulitibuka.

Aliposhindwa kuelewana na Inter, Icardi aliamua kuwacha kuwa nahodha wa timu hiyo na hilo likazua sokomoko baina yake na mashabiki. Hata hivyo, sasa hivi anaichezea timu ya PSG kwa mkopo.

4. Neymar (Brazil)

Miezi kadhaa tu baada ya kuteuliwa kama nahodha wa timu ya Brazil, shida zilimuandama kiungo huyu wa PSG na alishushwa cheo chake huku mkongwe, Dani Alves akiteuliwa.

Katika michuano ya Copa America, Brazil ambao hawakuonesha kukosa makali yake Neymar walijizatiti na kushinda kombe hilo.

5. Samuel Eto'o (Cameroon)

Licha ya kufungia nchi yake zaidi ya mabao 50 na kuishindia mataji mawili ya kombe la Africa, Eto'o hakuonesha mchezo mzuri katika kombe la dunia lililoandaliwa Brazil.

Kufuatia hilo, alishishwa cheo huku nafasi yake ikichukuliwa na Stephane M'Bia jambo lilopelekea yeye kustaafu kuichezea nchi yake akiwa na umri wa miaka 37.