WHO yaidhinisha majaribio ya dawa ya kienyeji iliyotengenezwa na taifa la Madagascar

madagascar-president
madagascar-president
Rais wa taifa la Madagascar Andry Rajoelina maesema kuwa shirika la afya duniani WHO limependekeza kufanyika kwa majaribio ya dawa ya kienyeji ambayo ilizinduliwa na taifa hilo.

Akizungumza na mkurugenzi mkuu wa WHO Dr Tedros Adhanom kupitia kwa njia ya video amesema kuwa Tedros amemhakikishia uungwaji mkono wa shirika hilo katika majaribio yake.

Taarifa hizi zinajiri siku chache tu baada ya kiongozi huyo wa Madagascar kuwarai wananchi wake kunywa dawa hiyo ya kienyeji kama njia ya kuzuia virusi hatari vya corona.

“Let’s drink this herbal tea to protect ourselves, to protect our family and our neighbours […] and there will be no more deaths,” Andry Rajoelina amesema.

Kufikia sasa kiziwa hicho cha kusini mwa Afrika kimesajili visa 304 huku watu waliopona kufikia sasa wakiwa watu 114 kulingana na data zilitolewa na chuo kikuu cha Hopkins nchini Amerika.

Maafa yaliyosajiliwa katika kiziwa hicho yalitokana na jamaa ambaye alikuwa anaugua ugonjwa wa kisukari.

Rajoelina amesema serikali yake inashirikiana na mataifa mengine na hata madaktari ili kuendeleza utafiti zaidi kubaini iwapo wanaweza kupata suluhisho linginde kwa janga hilo.

Kufikia sasa, Madagascar imetuma dawa hiyo ya kienyeji katika mataifa ya kiafrika kama vile viziwa vya Komoro, Jamhuri ya Congo, Liberia, Nigeria, Tanzania, Senegal na Chad.

Hata hivyo, WHO imeonya kuwa ni sharti wazingatie masharti ya madaktari kabla ya kuitumia.