Yaliyomo: Alivyotaka ufanyiwe mwili wake Tob Cohen. Itikadi za wayahudi zinasemaje?

sarah-wairimu-cohen-and-tob-cohen-e1568394290127
sarah-wairimu-cohen-and-tob-cohen-e1568394290127
Bwanyenye wa Uholanzi  aliyeuawa kinyama Tob Cohen alihakikisha kwamba alichotaka kifanywe baada ya kuaga kipo wazi.

Alitaka pia matakwa yake yaheshimiwe.

Mwili wa Tob ulipatikana katika tanki Kitisuru juma lililopita Septemba 13.

Alikuwa amefungwa kwa kamba shingoni na mikono kufungwa.

Soma hadithi nyingine:

Akizungumza na vyombo vya habari Jumapili ya tarehe 15, dadake Gabrielle Van, alifunguka kwamba familia ilikuwa tayari ishafanya uamuzi wa kumzika jijini Nairobi.

Hili lilikuwa pendekezo lake bwanyenye huyu.

Mwendazake alitaka mwili wake uzikwe katika makaburi ya kiyahudi yaliyopo barabara ya Wangari Maathai kabla masaa 48 kukamilika.

Walifanya misa takatifu kulingana na alivyoandika katika wasia.

Wasia ulisema kwamba mwili wake Tob usafishwe, ufunikwe na utayarishwe kwa mazishi kwa kufuata itikadi za kiyahudi.

Soma hadithi nyingine:

Msururu wa mahojiano na stakabadhi katika maktaba zilionyesha kwamba watu wanaotambulikana kama Shmira katika Torah walikuwa wanatazama mwili wake na kusoma zaburi au toba.

Hii ni mila na itikadi za dini ya Wayahudi.

Utamaduni vilevile ulimtaka awe ashatangaza kwa anaowapenda jinsi mazishi yatakavyoendeshwa.

Utaratibu wa mazishi ulipaswa kufuata itikadi za wayahudi.

Soma hadithi nyingine:

Alitakiwa azikwe katika itikadi za wale waliomtangulia Tob.

Sasa zoezi la kufanya upasuaji wa kutathmini kilichomuua bwanyenye huyu limehairishwa mpaka leo tarehe 18 Septemba.

Hii ni baada ya Sarah Wairimu kuomba daktari wake awepo katika zoezi hilo.

Wakili wa serikali Nicholas Mutuku aliiambia mahakama kuwa upasuaji huo ni ushahidi dhabiti utakaosaidia katika utatuaji wa kesi hiyo.

Upasuaji huu unatakiwa kufanyika leo katika eneo la kuhifadhi miili ya wafu Chiromo.

Mawakili wanaosikiliza kesi hiyo walikataa uwepo wa Dkt Peter Ndegwa katika zoezi hilo la upasuaji kwa misingi kwamba alitoa kauli kuhusu mwili huo pindi tu ulipatikana wiki iliyopita ijumaa.