Yaliyomo kwenye kapu la hotuba ya rais katika maadhimisho ya Madaraka day- Soma

Taifa la Kenya hii leo limeadhimisha miaka 57 baada ya kujinyakulia uhuru chini ya uongozi wa hayati Mzee Jomo Kenyatta. Na hii leo rais Kenyatta aliongoza taifa kuadhimisha maadhimisho hayo katika Ikulu ya taifa na kutoa ufafanuzi zaidi wa yale taifa la Kenya limeafikia tangu kujinyakulia uhuru na chini ya uongozi wake.

Kati ya maswala ambayo kiongozi wa taifa amegusia hii leo ni kufanyiwa katiba ya mwaka 2010 marekebisho ili kutatua changamoto za uongozi na kuleta usawa serikalini.

Kubaini hayo yote, soma baadhi ya mambo ambayo rais Kenyatta alizungumzia hii leo.

Viongozi wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni kiongozi wa ODM Raila Odinga, kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na mwenzake wa ANC Musalia Mudavadi.