Yaliyomo: Yalioyoandikwa A-Z katika wasia wa Tob Cohen, Sarah Wairimu hana kijisehemu

Mwendazake bwanyenye Tob Cohen aliyaacha maagizo yanayopaswa kufuatwa katika wasia kabla afariki.

Katika wasia huo, kakake na dadake wataurithi utajiri wake wa mamilioni.

Bwanyenye huyu ambaye ni raia wa uholanzi aliuawa kikatili na maafisa wa polisi wanadadisi tukio hilo.

Soma mengine hapa:

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (DCI) George Kinoti, ushahidi upo kwamba Cohen aliuawa katika boma lake mtaani Spring Valley na kisha kurushwa katika tanki.

Mtaalamu huyu wa huduma za ziara na usafiri katika wasia huo alikuwa ameandika kuwa wawili hao watamiliki sehemu iliyopo Kitisuru inayopiga hesabu ya milioni 400.

Mtaa wa Kitisuru ni sehemu inayojulikana kwa kuishi matajiri na wafanya biashara wakubwa.

Gazeti la uholanzi Algemeen Dagblad (AD) limenukuliwa katika vyombo vya habari kwamba dadake Cohen  Gabrielle van anahoji kuwa mipango ipo ya kumiliki sehemu hiyo juma lijalo.

Soma mengine hapa:

Gabrielle anasema kwamba alikuwa na nakala ya wasia wa kakake kwa muda.

Anadokeza kuwa hii ni njia salama Cohen alichukua kipindi na ambapo ndoa yake na Sarah Wairimu alivurugika.

Mwanadada huyu anasema kuwa kakake alihofia maisha yake sana hivyo akampa nakala ya wasia huo.

Wasia huo unasema kuwa Cohen angependelea kuzikwa nchini katika mila na itikadi za wayahudi.

Uchunguzi wa kina unaofanyika kwa sasa unaiweka familia katika wakati mgumu kufuata itikadi zao kwani mwili huo unafaa kuzikwa katika muda ya masaa 36.

“Tulijua kuwa alitaka azikwe Kenya...ila hatukujua wasia wake ulivyoandikwa." linasoma gazeti hilo.