Yawa! We are a poor economy. Total lock down itaangamiza wakenya - Gavana Mutua

NA NICKSON TOSI

Gavana wa kaunti ya Machakos Dr Alfred Mutua ametofautiana vikali na wale wanaomtaka rais Uhuru Kenyatta kusitisha kabisa shughuli zote nchini akisema ni hatari kwa taifa na hata huenda idadi ya wakenya wanaofariki kutokana na njaa ikaongezeka marudufu.

Mutua amesema serikali imekuwa ikishindwa kuwalisha wananchi wake wakati ambapo shughuli nchini huwa zinaendalea kikawaida na hivyo kuishurutisha serikali iyo hiyo kuwalisha wananchi wakati wa lock down ni kama kuchezea mbuzi gitaa.

Aidha Mutua ameongeza kuwa uchumi wa taifa kwa sasa umedorora pakubwa na iwapo rais Kenyatta ataamua kulifunga taifa basi wakenya wajitayarisha kwa maafa zaidi.

Mutua aidha amesema kuwa hatua ya serikali kufunga shughuli zote nchini ilichelewa na hivyo kuchukuwa hatua hiyo sasa itakuwa pigo kubwa .

Kuhusiana na iwapo kaunti yake iko na uwezo wa kufanyia watu vipimo vya virusi vya Corona Gavana huyo amesema hivi maajuzi hospitali kuu ya Machakos imeruhusiwa kufanyia watu vipimo na ina uwezo wa kufanyia watu 330-400 kwa siku.

Amesema hayo akiwa kwa mahojiano na kituo kimoja cha televisheni cha humu nchini