eliud-kipchoge_1

Yote utakayo kujua kuhusu bingwa Eliud Kipchoge

Eliud Kipchoge ni mwanariadha wa mumu humu Kenya ambaye bendera yake ya ugwiji katika mbio imepepea kweli kweli duniani kote.

kipchoge 5

Jamaa huyu ni gwiji kwani amebobea si kidogo na hata aliwashangaza wengi alipopata tuzo la kuwa mshindi wa mbio za Berlin na kuwa binadamu wa kwanza kabisa kumaliza mbio ile kwa dakika chache sana.

Eliud Kipchoge ni mzaliwa wa humu kenya Kaunti ya Nandi.

Kipchoge alizaliwa tarehe 5 mwezi wa 11 mwaka wa 1984 na kwa sasa ana miaka 34.

Bingwa huyu ana mke mmoja, jina lake Grace Sugut na pamoja wamebarikiwa na watoto watatu , vijana wawili na msichana mmoja ambao humwona baba yao kama kielelezo chema.

kipchoge wifeEliud.KIpchoge.Grace.Sugut.and.their.children

 

Familia ya Eliud inaishi jiji la Eldoret.

Katika mahojiano  na mke wake kitambo kidogo, mke wake alifunguka kuhusu siri ya mume wake kufaulu katika mashindano haya ya riadha na kusema kuwa bidii,nidhamu na kula chakula kizuri ndiyo siri ya mume wake kuwa mshindi.

Zaidi ya hayo, Grace Sagut alisema kuwa, mume wake ni mwanaume mtulivu na mnyenyekevu sana na huwa anaona wenzake jijini kama watu sawa-Maanake, huwa hajibagui na kuona kuwa yeye amefaulu zaidi maishani.

Vilevile, Eliud Kipchoge hurauka kila siku asubuhi kufanya mazoezi yake kwani ameeleewa fika kuwa, mtaka cha mvuguni sharti ainame.

kids kipchoge

Chakula akipendacho sana Eliud ni mahindi ya kuchoma, Ugali na maziwa ya mursik yaliyotengezwa na mke wake.

Vilevile, mke wake Eliud alisema kuwa, alimjua Eliud kutoka wakati ule walikuwa katika shule ya msingi mpaka shule ya upili na kwa sasa, wameishi katika ndoa kwa zaidi ya miaka 13.

Mke wake ndiye msaidizi wake katika mambo yote na hata husimamia biashara na mambo yote ya shamba kila wakati Eliud amesafiri kukimbia ama wakati ambao anafanya mazoezi.

Ama kwa hakika,ni wazi bayana kuwa Eliud na mke wake wanaishi maisha matamu sana ya wanandoa.

 

PICHA: Tazama jinsi Eliud Kipchoge alivyopewa mapokezi ya kifalme

Talanta ya Eliud ilianza akiwa katika shule ya msingi pale ambapo alikuwa anakimbia na kuwapiku wenzake wote.

Alipokuwa kwenye shule ya upili, aliendelea na mbio zile na kisha tu baada ya kumaliza masomo ya sekondari mwaka wa 1999, alikata kauli kufanya uwanariadha kuwa kazi yake .

Jamaa huyu alikuwa na mtu ambaye alikuwa anamtamanisha sana kuwa mwanariadha na kila wakati amuonapo, alipendela sana kuwa kama yeye.

Patrick Sang aliyekuwa mshindi wa medali ya fedha wa mashindano ya IAAF ndiye aliyekuwa mwanaridha ambaye Eliud alitamani sana kuwa kama na hata akamuomba bwana Patrick kuwa kocha wake.

kipchoge coachkipchoge 6

Patrick ambaye pia ni jirani yake Eliud kule nyumbani alikubali wito huu na sasa ni zaidi ya miaka 16 kufanya kazi na kumkochi Eliud Kipchoge.

Licha ya hayo, Eliud Kipchoge alisema kuwa, bwana Patrick si kocha wake wa michezo pekee bali pia ni kocha wake wa maisha.

Masaibu ya Man United na Tottenham, shida ni kocha ama wachezaji?

Vilevile, Eliud husema kuwa, kukimbia ni kama vile kusafiri kwa muda mrefu na kuzidi kusema kuwa kinachomsaidia ni kuweka akili yake alipo wakati anakimbia na kuzingatia mbio kwani wahenga walisema,njia mbili zilimshinda fisi.

kipchoge 4

Eliud alifunguka zaidi na kusema kuwa, yeye hujiamini na hufanya mazoezi ya kutosha kila wakati kabla ya  kuenda kwenye mashindano yoyote ya mbio.

Zaidi ya hayo,Eliud anatumai kuwa siku moja kenya itakuwa nchi ya wanariadha na kuwa wanariadha inamaanisha kuwa wakenya  itakuwa na watu wenye afya nzuri na nchi itakuwa nchi tajiri.

kipchoge.training

Vilevile, Eliud anasema kuwa watu wanafaa kuwa na uraibu wa kukimbia kama njia ya kuwa na afya nzuri na si tu kama kazi ya uwanariadha huku akitoa mfano wa kampuni fulani aliyozuru ambapo kila mtu kwenye kampuni hiyo alitakiwa kukimbia kilomita 5 kila alhamisi.

Eliud alisema kuwa wafanyikazi hawa waliweza kutoa mazao zaidi na hata wakawa wenye afya bora.

Mbali na kufanya mazoezi, Eliud anapenda sana kusoma vitabu.

Kwa sasa, Eliud amesafiri mji  ya Vienna kwa mbio ambazo anatarajiwa kukimbia chini ya masaa mawili na sisi kama Radio Jambo, tunamtakia kila la heri katika mbio hizo.

EGUrV3ZXkAAe3O9-compressedeliud kipchogekipchoge

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments