Mildred odira

Yuko wapi mfanyakazi wa nation media group Mildred Odira

Familia ya mwanamke ambaye anafanya kazi katika nation media group, ambaye anafanyakazi kama (switchboard operator) walitaka msaada wa kumtafuta mfanyakazi aliyepotea.

Habari za Nairobi zinatuarifu kuwa Mildred Odira alionekana mara ya mwisho jumanne asubuhi akitoka nyumbani kwake na gari ya texi.

I have lost two sons, survived toxic relationship, three types of cancers and 13 operations – Agallo

Mlinzi katika makazi ya Mildred Kariobangi South alieleza kuwa mama huyo wa mtoto mmoja, aliweza kuita texi ili kuenda hospitali ya Ruaraka Uhai Nema kwa kuwa mgonjwa usiku huo.

Imebaki kuwa kitendawili kwa familia ya Mildred kwa maana hawana habari zozote alipokuwa, na hali yake iko vipi.

Dadake Maureen Anyango alisema kuwa wameenda hospitali tofauti kumtafuta dadake, lakini bidii yake imeambulia patupu.

Mildred odira

Anyango alifichua kuwa dadake alikuwa na ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu na pia vidonda vya tumbo huku akiongezea kuwa aliweza kuzungumza na Mildred jumatatu ili kumjulia hali yake.

Wafanyakazi wenza wa Odira walisema wazi kuwa walimuona mwisho Alhamisi kwa sababu ijumaa aliweza kuchukua siku ya mapumziko ili aweze kuenda kumuona daktari ama kupokea matibabu.

Hata hivyo baada ya kutembelea au kuenda hospitali, madaktari waliweza kumjulisha Mildred kuwa shinikizo la damu yake iko chini sana na kumuambia arudi tena jumatatu kwa upimaji zaidi.

Anyango alisema kuwa alijua dadake hayuko wakati mtoto wa Mildred alipoenda nyumbani kwake.

Gidi mourns death of legendary musician Ayub Ogada

“Tulimuona mvulana wake akikuja nyumbani kwangu kisha nikamuuliza kwanini hajaenda shule,

“Aliniambia kuwa Mildred alitoka asubuhi na mapema na hapo ndipo niliweza kuulizia alipokuwa na kujua alienda wapi,” Alielezea Anyango.

Aliweza kumpigia simu ili kumjulia hali lakini hakuweza kuzungumza na yeye kwa maana simu yake ilikuwa imezimwa.

Baada ya kutompata kupitia kwa njia ya simu, alienda nyumbani kwake mahali dereva wa texi alimchukua asubuhi.

Kwa muda waliweza kuzungumza na dereva huyo na kusema alifikisha Mildred hospitalini na kumuacha baada ya dakika 20.

Hata hivyo kamera za CCTV zinaonesha dereva huyo akiingia katika hospitali hiyo saa 4:30 asubuhi na kisha kutoka saa 5:57 asubuhi.

Katika hali hiyo ya kumtafuta Mildred, je dereva anasema ukweli? ilhali anaonekana amemaliza zaidi ya dakika 20 alizosema.

Na anajua alipo Mildred? ni maswali ambayo familia inajiuliza na kugonga katika akili zao.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments