Yusuf Juma Apeana Masharti Ambayo Wapendanao Wapaswa Kufuata Siku Ya Valentine's (AUDIO)

Imekuwa mda mrefu kabla bwana Yusuf Juma azungumze hewani licha ya kusoma habari kila asubuhi katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi.

Hii leo ikiwa siku ya wapendanao, mwanahabari huyo aliamua kuwapa wapendanao mawaidha au masharti wanayopaswa kufuata huku wakijipanga kusherehekea siku hii ya kipekee.

Kulingana na Juma, haya ndio masharti ambayo wapendanao wafaa kufuata kabla ya vitu kuharibika.

  1. Hufai kuahidi au ku propose siku ya Valentine's. Kitu unachofaa kufanya ni kitu ulichokuwa umekipanga tangia mwaka uanze.
  2. Siku ya Valentine's ndio siku wafaa kuzugumzia uhusiano wako na mpenzi wako na pia kuelezea maazimiano.
  3. Unafaa kuwa muangalifu kwa mtu ambaye unamnunulia zawadi kwani aweza kuwa mwanadada au mwanaume aliyeolewa.
  4. Hufai kutumia fedha kupita kiasi.
  5. Usinunue zawadi kipindi cha lala salama kwani kuna uwezekano wako kununua zawadi isiyofaa.

Skiza kanda ifuatayo.