Kulikuaje? Msanii YY asimulia vile alivyokuwa mcheshi

YY
YY
YY almaarufu Oliver Otieno alizaliwa katika kaunti ya Homabay, kisha akalelewa katika kaunti ya Nairobi.

Alipenda sana kupika na kusafisha nyumba.YY aliweza kumpoteza baba yake akiwa bado shule huku wakibaki na mamake wa kuwakimu na ndugu wake watatu.

Mcheshi YY ni kifungua mimba katika familia yao, amemuacha ndugu yake anaye mfuata na miaka 8 na yule mwingine miaka 10.

"Nilipenda kupika kuosha nyumba kwa maana mamangu  alikuwa mwanabiashara. Mama alikuwa mwanabiashara, kwa hivyo alikuwa anapata nimepika alafu wakati huo kulikuwa na 'polythene paper'.

"Sasa nilikuwa napika alafu nafunika chakula na hayo makartasi," alisema YY

Oliver alikuwa anapika akitoka shule saa saba kisha anapika na kuandaa chakula cha usiku.

"Babangu alikuwa saa zingine anakuja nyumbani akiwa amelewa kisha anaanza kumpiga mamangu, hapo ndipo uusiano wangu na mamangu uliweza kukuwa kwa sana."

YY alisema kuwa amemuacha ndugu yake anaye mfuata kwa miaka 8 kwa sababu yeye ndiye kifungua mimba kwa familia yao.

Aliweza kusema kuwa ana mchumba ambaye wamechumbiana kwa mwaka mmoja sasa.

Baba Oliver alipofariki alikuwa anaona maisha yakiwa magumu na kuanza kufikiria kuwa kama babake angekuwa mambo yangekuwa rahisi.

Wakati huo huo anafikiria mateso ambayo babake alifanya mamake apitie. YY alisema kuwa wanawake hawafai kudhulumiwa wala kuteswa lakini wanapaswa kuishi huru.

Ata kama  baba yao alikuwa anatesa na kumchapa mama yao alikuwa ana wapenda sana. Hapo ndipo aliweza kukua akijua kuwapa heshima wanawake.

Watoto wa baba yake ni wawili lakini baada ya baba yake kuaga mama yake aliweza kuolewa na kupata mtoto wa tatu ambaye ni msichana na anampenda sana, licha ya mama yake kupitia hayo yote.

"Nilianza ucheshi shuleni na kanisani. Nilipomaliza kidato cha nne nilijiunga na chuo kikuu cha Kenyatta kusomea (medical statistics)yaani takwimu za matibabu,

"Ndipo nikajiunga na (Kenyatta university traveling theater)"Alisema YY.

YY akijiunga na chuo kikuu alikuwa anataka kuwa meneja wa huduma za afya kwa kimombo (health service manager).

"Niliweza kua MC kisha rafiki yangu alinishauri niweze kujiunga na Churchill Show. Kesho yake nilipelekwa na rafiki yangu Lawrence Carnivore kwa mguu ili nikachaguliwe kama mcheshi.

"Lakini nikaanguka lakini si kufa moyo nilirudi tena na tena hadi wiki ya 4. Kitendo kilicho fanya nifukuzwe na mjomba wangu nyumbani kwa kusimamisha masomo yangu lakini sikurudi nyumbani nilirudi tena Carnivore kisha nikaweza kuchukuliwa."aliongezea YY.

&feature=youtu.be