Zambia yaamua! Imefunga mipaka inayoingia katika taifa hilo na taifa laTanzania

Nakonde-730x414
Nakonde-730x414
Taifa la Zambia limekuwa la hivi karibuni kufunga mipaka yake na Tanzania baada ya kusajili visa vingi vya maambukizi ya corona Wikendi hii.

Huku taifa hilo likiendelea na juhudi za kuwapima watu, Zambia ilisajili visa 85 vipya vya maambukizi ya virusi hivyo Jumamosi hatua ambayo iliipelekea kuchukua hatua hiyo.

Kulingana na taarifa zilizochapishwa na The Citizen, visa 76 vilitokea katika maeneo ya Nyakonde, eneo ambalo linapakana na Tunduma Tanzania.

Waziri wa afya wa taifa hilo Chitalu Chilufya amesema watafunga mpaka huo ili kupunguza idadi ya maambukizi ya virusi hivyo.

“No traffic will be allowed in and out of the district,” Dr. Chilufya alisema.

Kwa kuwa mataifa yote mawili ni wanachama wa muungano wa kibiashara wa SADC, Chilufya alisema ni sharti hatua za haraka kuchukuliwa ili kupunguza usambaaji wa virusi hivyo.

Haijabainika wazi ni lini marufuku hayo yatakapoisha japo waziri huyo amesema iwapo maambukizi katika mpaka huo yatapungua, basi watalazimika kuufungua.