Zari asimuluia jinsi gavana Mike Sonko anavyo msisimua

Aliyekuwa mpenziwe Diamond Platinumz, Zari Hassan, amesema kuwa yuamtamani gavana na Nairobi Mike Sonko na angependa sana kupatana naye kabla ya mwaka kuisha.

Akizungumza na kituo kimoja cha habari nchini Africa Kusini, Zari alisema,"Ningependa kulionesha penzi langu kwa gavana wa Nairobi Mike Sonko aliye mtanashati kwelikweli. Ndiye mwanaume ambaye nuimekuwa nikitamani kisiri kwa muda mrefu ."

"Nampenda gavana huyu kwa kuwa yeye ni mwanaume aliye na utu uzima pamoja na tabia za kupendeza. Sonko sio kama hawa wavulana wadogo wadogo ambao wamekuwa wakinifuatafuata hapa na pale."

Zari amesema kuwa Sonko anamkumbusha aliyekuwa mumewe Ivan aliyaga dunia.

"Mkimwona Sonko tafadhali mwambieni kuwa kuna mtu anayemjali. Nampenda kwa sababu licha ya kuwa na uwezo mkubwa, yeye anafanana na marehemu bwanangu Ivan aliyependa kuwasaidia maskini," Zari alisema.