Zari Hassan apata kipenzi kipya

Baada ya ukimya wa muda mrefu, Zari ameweza kutokea katika mitandao ya kijamii na mwanaume ambaye amtamrithi msanii na mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz. Katika chapisho siku ya ijumaa, mrembo huyu na mama wa watoto watano amesema kuwa mwanamume aliyempata kwa sasa ni baraka kubwa kwake.

Zari na Diamond waliachana mwaka uliopita tarehe 14 Februari siku ya wapendanao kwa kuchapisha ua jeusi lililoambatana na ujumbe mzito wa kuonyesha hawapo tena katika mahusiano.

Anasema Bwana M ni tofauti na wapenzi wa jadi na kwamba ana upole na utulivu mwingi ambao unafanya ampende zaidi. Mzazi mwenza Simba  anaonekana kuzama katika mahaba mazito na mtangazaji wa redio Tanasha Donna kutoka hapa nchini.

Penzi lake diamond na Tanasha linaonekana kunoga zaidi baada ya mkali huyu kumpeleka Donna nyumbani Madale na kumtambulisha kwa  familia. Dadake Platnumz anapenda sana mahusiano haya na anajuta kuwa wawili hawa wangekutana zamani.