Zidane: Lazima Bale aondoke Madrid

tammy-abraham-1068x580
tammy-abraham-1068x580
Kocha mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema kuwa anatarajia mshambulizi wake Gareth Bale kuigura klabu ya Real Madrid msimu huu.

Zidane akizungumza na vyombo vya habari baada ya mechi baina ya Real Madrid na Bayern Munich, alisema kuwa Bale hayupo kwenye mipango yake ya msimu ujao.

Ajenti wake Bale Jonathan Barnette kwa upande mwingine, amemkashifu Zidane kwa kumfukuza Bale ugani Santiago Bernabue.

Mshambulizi mpya wa Barcelona Antoinne Griezmann amesema kuwa itakuwa vigumu kwa Fc Barcelona kukamilisha uhamisho wake Neymar Kutoka klabu ya PariS Saint Germain ya Ufaransa.

Griezmann alikamilisha uhamisho wake wiki iliyopita kujiunga na Barcelona huku kukiwa na uvumi kwamba Neymar atajiunga na wahispaniola hao hivi Karibuni.

Mshambulizi wa Chelsea, Tammy Abraham amesema yupo tayari kuonyesha uwezo wake kwenye kikosi cha kwanza msimu ujao.

Abraham anatarajiwa kuwania nafasi katika kikosi cha Kwanza cha Chelsea pamoja na Michy Batshuayi.