Zimemshika mbayaa! Betty Kyallo azusha akiwa mlevi kwenye video Instagram

NA NICKSON TOSI

Wee! Nani aliyesema hustahili kunywa na kuendesha gari? Basi mwambieni aongeze kuwa hustahili kufanya video katika mitandao ya kijamii ukiwa mlevi .

Betty Kyallo, mwanahabari anayefahamika sana kutokana  na kashfa nyingi za uhusiano baina yake na Dennis Okari amewaacha wengi vinywa wazi baada ya kufanya video katika mtandao wake wa Instagram na kuwashambulia wanablogu wanaopenda kuandika taarifa kuhusiana na maisha yake.

Betty aliwakashifu wanablogu hao kwa kuingilia maisha yake ya kibinafsi na kuandika taarifa ambazo zinamfanya kukosa ladha ya kusherehekea maisha yake.

Betty amekerwa akikashifiwa kuhusiana na mienendo yake ya kuenda kwenye klabu usiku wengi wakisema kuwa haonyeshi kielelezo chema kama mama na kwa mwanawe msichana Ivanna.

Kulingana na wakosaoji wake, Betty anastahili kupunguza safari zake za kujivinjari kwenye klabu na kuishi maisha ya heshima kama mtu anayetazamiwa na wengi kwenye jamii.

Hapa ni baadhi ya maoni ya wafuasi wake

fungua roho betty

Si unakaa poa ukilewa🤣🤣
Leo ni leo Betty 🤣🤣🤣🤣🤣🤣😍😍❤
Life is too short to stay serious always 😂😂❤