Zoezi la kutafuta stakabhadhi za Sharon na Melon laanzishwa

twipic
twipic
Wahudumu katika hospitali kuu na ya rufaa ya Kakamega jana jumapili wamejikita katika mchakato utakaokuwa mgumu wa kutafuta kumbukumbu na stakabadhi za tangu miaka 19 iliyopita. Mkurugenzi wa maswala ya afya kaunti hiyo, Rachael Okumu amewaagiza wafanyakazi katika kituo hicho cha matibabu kutafuta stakabadhi zinazoonyesha Sharon na Melon walizaliwa katika hospitali hiyo.  Hii ni baada ya uchunguzi wa msimbojeni au DNA kuonyesha kuwa Sharon Mitekwa na Melon Lutenyo ni mapacha waliozaliwa na mama mmoja.

Soma hapa:

"Tunajitahidi kutafuta kumbukumbu zetu ili tujue Sharon na Melon walizaliwa lini. tunajitahidi pia kujua kitu gani haswa kilichangia kutengana kwao." alisema mhudumu mmoja.

Inaaminika kuwa mapacha hawa walitenganishwa miaka kumi na tisa iliyopita katika hospitali hiyo. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa ustadi mwingi na shirika la Lancet Kenya (PLK) na kuchapishwa jumamosi, Sharon na Melon ni mapacha kamili asilimia mia.

Pata uhondo zaidi:

Uchunguzi huo wa kina pia unaonyesha kuwa Rosemary Onyango ndiye mama wa mabinti hawa. Kisa hiki kiliwavutia na kuwashangaza wakenya mwezi wa Aprili. Wengi walihoji kuwa mabinti hawa walikuwa mapacha kwa kuwa walifanana sura zao.

Angeline na Rosemary walitemblea kituo hicho cha matibabu wakati mmoja na inakisiwa kosa lilifanyika wakati huo wa kujifungua. Baada ya takriban miongo miwili, mabinti hawa walipatana katika mtandao wa kijamii wa Facebook huku wakishangazwa na jinsi wanavyofanana kama shilingi kwa ya pili. Walipanga kukutana huku swala hili.