Tazama maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme Jumanne

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Aprili 30.

Muhtasari

•KPLC Ilisema baadhi ya maeneo ya kaunti 8 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na   Nairobi, Kiambu, Makueni, Busia, Kisii, Homa Bay, Nyeri, Laikipia.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Aprili 30.

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema baadhi ya maeneo ya kaunti 8 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na   Nairobi, Kiambu, Makueni, Busia, Kisii, Homa Bay, Nyeri, Laikipia.

Katika kaunti ya Nairobi,baadhi ya sehemu za maeneo ya Zimmerman, Mathare, Ruaraka, Siaya Road, Donholm, na Savannah zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za mji wa Limuru, na kiwanda cha Carbacid katika kaunti ya Kiambu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Mji wa Wote katika kaunti ya Makueni pia utaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Busia, baadhi ya sehemu za maeneo ya Malaba, Amagoro na Kocholia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za mji wa Kisii katika kauti ya Kisii zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa moja asubuhi na saa nane mchana.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Ringa, Ramula, na Mawego katika kaunti ya Homa Bay zitakosa umeme ya kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Katika kaunti ya Nyeri, sehemu kadhaa za maeneo ya Ngaru na Kariko zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Timau, Kiambogo, na Ethi katika kaunti ya Laikipia pia zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.