KPLC yatangaza maeneo yatakayokosa stima leo, Jumanne

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Aprili 23.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Aprili 23.

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Nairobi, Kiambu, Nyeri na  Kilifi.

Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za maeneo ya Riverside na Githogoro zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za eneo la Karura katika kaunti ya Kiambu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Ringroad na Ngangarithi katika kaunti ya Nyeri pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za eneo la Mtondia katika kaunti ya Kilifi pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.