Ruto aahirisha kufunguliwa kwa shule kwa muda usiyojulikana

Tarehe ya awali ya kufungua shule ilikuwa imesukumwa kutoka Jumatatu 29 Aprili hadi Jumatatu Mei 6.

Muhtasari

• Rais William Ruto ameagiza Wizara ya Elimu kuahirisha kufunguliwa kwa shule zote hadi pale serikali itaona ni salama kufanya hivyo.

Rais Ruto kuongeza idadi ya watoza ushuru kwenye masoko, mitaa.
Rais Ruto kuongeza idadi ya watoza ushuru kwenye masoko, mitaa.
Image: Facebook

Rais William Ruto ameagiza Wizara ya Elimu kuahirisha kufunguliwa kwa shule zote hadi pale serikali itaona ni salama kufanya hivyo. Rais alitoa agizo hilo siku ya Ijumaa wakati wa hotuba yake ya kitaifa. 

“Wizara ya Elimu imeagizwa kuahirisha tarehe za kufunguliwa kwa shule zote nchini kwa muhula wa pili hadi itakapotangazwa tena,” Rais alisema. 

Tarehe ya awali ya kufungua shule ilikuwa imesukumwa kutoka Jumatatu 29 Aprili hadi Jumatatu Mei 6.