Watu mashuhuri wanaopendwa zaidi na Gen Z

Utafiti huo ambao ulikusanya majibu kutoka kwa vijana 1300 wenye umri wa miaka 18-27, ulimweka TikToker Azziad Nasenya juu ya orodha ya watu mashuhuri wanaopendwa

Muhtasari
  • Linapokuja swala la wanasiasa, kiongozi wa Azimio Raila Odinga aliibuka kuwa mtu anayependwa zaidi, huku rais William Ruto na mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino wakifuata mkondo huo.
Lulu hassan na Eric Omondi
Image: Instagram

Utafiti wa hivi punde umeangazia mapendeleo ya kizazi kipya cha Gen z nchini Kenya, kikionyesha kuvutiwa sana na watu mashuhuri wa ndani na mwelekeo thabiti wa mitandao ya kijamii kama njia ya taaluma.

Utafiti huo ambao ulikusanya majibu kutoka kwa vijana 1300 wenye umri wa miaka 18-27, ulimweka TikToker Azziad Nasenya juu ya orodha ya watu mashuhuri wanaopendwa na kufuatiwa na mcheshi Eric Omondi.

Azziad Nasenya
Image: Facebook

Mtangazaji wa habari Lulu Hassan na mwimbaji Otile Brown pia walikuwa miongoni mwa waliopendwa zaidi, na kupata nafasi ya tatu na ya nne mtawalia.

Linapokuja swala la wanasiasa, kiongozi wa Azimio Raila Odinga aliibuka kuwa mtu anayependwa zaidi, huku rais William Ruto na mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino wakifuata mkondo huo.

Rais wa zamani Uhuru Kenyatta na Martha Karua walikamilisha watu 5 wakuu wa kisiasa.

Ukuaji wa mitandao ya kijamii umeathiri matarajio ya kazi miongoni mwa vijana huku 75% wakionyesha nia ya kupata umaarufu na kuzingatia kuwa waundaji wa maudhui, wanablogu, au washawishi kama taaluma halali na ya kupendeza.

Hasa, utafiti wa Odipo dev na Afrika uncensored , ni chombo huru cha uchunguzi ambacho kilifichua kuwa wanne kati ya 5 Gen Z wangeiacha Kenya na kwenda nchi za kigeni ikiwa fursa hiyo itatokea.

Wale waliotaka kuhama, 80% walichagua Marekani kama wanakopendelea, huku 60% wakichagua Ulaya.

Australia pia iliorodheshwa juu kwenye orodha, ikiwa na idadi kubwa ya wahojiwa wanaotaka kuishi katika nchi za Asia au ndani ya Afrika Mashariki lakini nje ya Kenya.