logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanahabari Miss Mandi achaguliwa Youtube Black Voices Fund

Mwanahabari wa redio, Miss Mandi amechaguliwa katika hazina ya YouTube Black Voices Pamoja na Wakenya wenza watatu ambao ni Justus, Wendy Angel na Cheyenne Muvunyi, wote hawa wakiwa ni wanablogu katika mtandao wa YouTube.

image
na Davis Ojiambo

Burudani28 January 2022 - 11:58

Muhtasari


  • • Mwanahabari wa redio, Miss Mandi amechaguliwa katika hazina ya YouTube Black Voices Pamoja na Wakenya wenza watatu ambao ni Justus, Wendy Angel na Cheyenne Muvunyi, wote hawa wakiwa ni wanablogu katika mtandao wa YouTube.
Instagram

Mwanahabari wa redio, Miss Mandi amechaguliwa katika hazina ya YouTube Black Voices Pamoja na Wakenya wenza watatu ambao ni Justus, Wendy Angel na Cheyenne Muvunyi, wote hawa wakiwa ni wanablogu katika mtandao wa YouTube.

Ushindi huu unajiri wiki mbili tu baada ya habari za Miss Mandi kusambazwa na kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii katika kile ambacho wengi walimtaja kuwa mnyanyasaji wa kijinsia haswa kwa wafanyakazi wenza.

Akizungumzia ushindi huu mkubwa, Miss Mandi ameweka kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema kwamba ana furaha sana kuwa miongoni mwa wale waliochaguliwa.

“Ninajihisi niko mwezini nikibarizi katika baraka zangu. Nina furaha sana kuwa miongoni mwa kundi la YouTube Black Voices kwa mwaka wa 2022. Ninatazamia kuinua na kuongeza maudhui yangu, kukuza jamii na kufanya mambo ya ngazi za juu kabisa,” aliandika Mandi.

Hazina ya YouTube Black Voices ilibuniwa ili kuwasaidia moja kwa moja wasanii weusi wanaokukuza maudhui mitandaoni ili pia nao wapate mafanikio na ustawi katika mtandao huo mkubwa wa video.

Licha ya kupakwa tope kama mwanamke mwenye ukatili katika mazingira ya kazi na wakenya wengi, Miss Mandi amepokea jumbe za hongera na sifa kochokocho mitandaoni kwa ushindi huo mkubwa.

Hongera sana Miss Mandi!


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved