Kasisi John Pesa ambaye mahubiri yake yalihusisha usemo kwamba Solomon ndye aliyemua Goliath akiwa katika ziara ya viongozi wa kidini kutoka Nyanza kwa naibu wa rais William Ruto huko Sugoi amedai kwamba maisha yake yamo hatarini
Pesa ambaye alilenga kumhusisha Ruto na David ambaye alimwuua Goliath katika Biblia aliteleeza na kusema kwamba ni Solomon ndiye aliyemua Goliath hatua iliyozua sana mhemko katika mitandao ya kijamii na kila aliyekuwa akitazama mahubiri yake .
"Mimi ni mzee sana..sikumanisha nilivyosema. Nasikitika kwamba watu wangali wanaendeleza ptyovu huo kuhusu nilichosema’ amesema Pesa
Pia amedai kwamba maisha yake yamo hatarini baada ya ziara yake kumuona Ruto . Mhubiri huyo amesema tangu walipomtembelea Ruto amekuwa akipokea jumbe za vitisho huku baadhi ya watu wakija kwake awape pesa ambazo wanasema alipewa na Ruto
Amesema ameripoti tukio hilo katika kituo cha polisi cha Kondele huko Kisumu .Pesa amekanusha kupewa fedha wakati wa ziara hiyo
"Ruto ni hasla na hana pesa’ amesema
Hata hivyo kulingana na gazeti la Taifa Leo kassi huyo alidai kupewa shilingi elfu kumi pekee wakati wa ziara hiyo nyumbani kwa Ruto
Ameliambia gazeti hilo kwamba kati ya pesa hizo alitumia shilingi 6000 kuweka mafuta kwenye magari yake mawili kwa safari ya kutoka Kisumu hadi sugoi na kusalia na shilingi 4000 pekee .
Amedai kwamba aligundua kwamba viongozi wengine wa makanisa waliokuwa katika ujumbe huo walipewa kiasi cha juu cha pesa kuliko shilingi elfu kumi ambazo yeye alipewa .
‘ Hilo linafaa kulaaniwa sana ,pesa kama hizo hazifai kupewa watu kwa njia ya ubaguzi’ amesema Pesa