Naibu wa rais William Ruto amezifariji familia zilizwapoteza watu 10 baada ya boti waliomokuwa wakisafiria kuzama katika ziwa Victoria .
" Ni jambo la kuhuzunisha kwamba tumewapoteza wakenya katika ajali ya boti ziwani Victoria .rambi rambi zangu ziwaendee watu wa familia zilizowapoteza wapendwa wao huko Siaya’ amesema Ruto
Mwenyekiti wa usimamizi wa Ufuo katika eneo ambako ajali hiyo iliyokea Elly Odhiambo Masinde amesema boti hiyo ilikuwa imewabeba watu 20 ilipozama majini kwa sababu ya upepo mkali .
Amesema watu kumi walikufa maji ilhali wengine kumi waliokolewa wakiwemo watu 9 wazima na mtoto mmoja aliyeokolewa na wavuvi .
Naibu wa chifu wa Got Agulu Fredrick Ochieng amesema shughuli ya kuiondoa miili hiyo majini inaendlea .Ameitaka serikali kuwapa msaada katika opareshei hiyo .
Mwili wa mwanamme mmoja umeshapatikana hadi kufikia sasa . oparesheni hiyo inaendeshwa na wavuvi wa eneo hilo ,kundi la usimamizi wa ufuo na maafisa wa Kenya Coast Guard
Ripoti zasema maafisa wa usalama wa majini wanawasiliana na Uganda ili kusafirisha mwili kwa marehemu hadi Uganda . Gavana wa Siaya Cornel Rasanga pia ametuma risala za rambi rambi kwa familia zilipatwa na mkasa huo .Rasanga ameahidi kuzisaidia familia ziliwapoteza wapendwa wao na zile ambazo miili ya jamaa zao haijapatikana .