Muigizaji wa Filamu za Bongo Wema Sepetu ametoa maoni yake kuhusu bango lililowekwa na mwanadada moja akisherehekea mume wake siku ya wapendanao.
Wema amepenndezwa sana na video hiyo ambayo imewavutia zaidi wanamitandao huku akisifia mwanadada aliyeweka bango hilo kudhihirisha mapenzi yake kwa mumewe.
Haya yametokea baada ya video iliyokuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mwanadada aliyeweka kipenzi chake cha roho kwenye bango kubwa na kuliweka kando ya barabara ili dunia inaposherehekea Valentine's.
Hisia mbalimbali zilitolewa kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakisifia mapenzi ya mwanadada huyu kwa mumewe.
Wema Sepetu hakusazwa nyuma huku akizamia kwenye ukurusa wake wa Instagram kupakia video hiyo na kuwatakia wapenzi husika ndoa yenye furaha.
“Naomba nimalizie na hii apa, Na mimi ipo siku nataka kuwa kama wewe. Hii ndio njia nzuri kuonyesha kweli unapenda mtu… wenzangu na mimi naoba tutulie,kama hujamuweka kwa bango basi sio valentine wako.. Allah abariki penzi lenu,” alisema Wema
Vilevile, video hiyo ilionekana kama kumrejesha nyuma wakati mapenzi baina ya Diamond na Wema yalikuwa ya kupigiwa mfano