logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Askofu akwepa kuchomwa moto kwa kutoroka na pesa za siasa

Askofu Yegon alipewa pesa na Charles Keter kugawia watu lakini akatoroka nazo

image
na Davis Ojiambo

Burudani24 March 2022 - 06:52

Muhtasari


  • • Askofu maarufu katika kaunti ya Kericho aliponea kifo cha kuchomwa moto kwa ghadhabu ya wananchi baada ya kujaribu kutoroka na pesa za kampeni kisiasa.
Picha ya Askofu Yegon akikimbilia maisha yake baada ya ghadhabu ya wananchi

Askofu maarufu katika kaunti ya Kericho aliponea kifo cha kuchomwa moto kwa ghadhabu ya wananchi baada ya kujaribu kutoroka na pesa za kisiasa ambazo mwanasiasa mmoja alimkabidhi kugawia wananchi.

Kulingana na mwanablogu maarufu Abraham Mutai ambaye pia alisambaza video ya tukio zima, Askofu huyo kwa jina Yegon alicheza kitenesi na kifo baada ya kufanya ubahili wa kutoroka na pesa ambazo Waziri wa kawi Charles Keter, ambaye anawania ugavana wa kaunti ya Kericho alimpa ili ashiriki pasu kwa pasu na watu wa eneo hilo.

Mtumishi wa Mungu alionesha watu mchezo wa kufana baada ya kudhihirisha uwezo wa miguu yake kumponya na kudakia bodaboda moja iliyokuwa karibu na kisha kukwepa kifo cha moto baada ya mambo kuenda mrama.

Inadaiwa watu wengi walimchagua mhubiri huyo kukabidhiwa pesa hizo kwa kumuamini kwamba yeye ni mja wa Mungu na hawezi kuwatapeli lakini pindi bunda la noti lilipotua viganjani mwake, ghafla ibilisi akamkonyeza kwamba ni wakati wa kuonesha picha zake kamili na kidhihirishia umma uwezo wa miguu yake.

Haya yanajiri huku kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti zikianza kupamba moto na mkoko kualika maua ambapo wanasiasa mbalimbali wameanza kujitafutia umaarufu kwa gharama zote ikiwemo kutumia pesa kwa wananchi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved