logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu wapagawa kwa rangi ya ngozi ya mtoto wa Nandy

Watu walisema kwamba rangi ya ngozi ya mtoto huyo haina ushabihiano wowote na wazazi wake.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 April 2023 - 06:54

Muhtasari


  • β€’ β€œMimi unanichanganya buanaaa rangi yetu sio hii,” Ammy Gall Tz alimwambia.
Nandy aonekana na mtoto wake kwa mara ya kwanza.

Kwa mara ya kwanza msanii Nandy amepakia picha akionekana na mwanawe.

Msanii huyo amnbaye alijifungua mwaka jana amekuwa akipakia picha zake yeye na mume wake huku sura au hata picha ya kuonekana na mtoto ikisalia kuwa ndoto tu, lakini safari hii angalau amewapa mashabiki wake sababu ya kuamini kama kweli yeye ni mama.

Nandy alisema kwamba mwezi wa Aprili ndio mwezi wa shughuli yake kuu, akiwaomba wafuasi wake kutoa takwa moja kati ya kuwaonesha sura ya mwanawe au kufichua jinsia.

Lakini gumzo kubwa halikuwa katika yeye kuonekana na mtoto maana wengi tayari walikuwa washajua alishazaa, gumzo kubwa lilijikita katika rangi ya ngozi ya mtoto huyo.

Wengi walibaini kwamba mtoto yule alikuwa na rangi nyeusi kidogo ambayo ni tofuati na Nandy na mumewe Billnass ambao wote angalau wana rangi ya hudhurungi kwa mbali.

Hilo lilifanya baadhi kuhisi kwamba Nandy aliwapiga changa la macho, wakisema mtoto huyo aliyeonekana naye si wake bali ni wa mtu alitaka tu kupiga picha naye ili kuzima uvumi ulioko mitandaoni kwamba hana mtoto.

Mimi unanichanganya buanaaa rangi yetu sio hii,” Ammy Gall Tz alimwambia.

“Huyuu sio mtoto wako usitudanganye kwanza uyoo ni WA kiume hilo tangazo la shughuli zetu kwa watu ila sio wa kwako huyo,” mwingine alimwambia.

“Mtoto hajatuangusha kwenye rangiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ wana sifa hawa viumbe πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ mi nusu nilie hospitali,” mwingine alisema, akionekana kudokeza kwamba watoto wakati mwingine huja kwa kutowafanana kabisa wazazi.

“Watu ukubwani wanajichubua ona sasa mtoto katoka na rangi yenu ya zamaniπŸ˜’ sijui rangi ya old skuliπŸ™” huyu alimpiga makombo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved