logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nimepitia maisha magumu, sifanyi bidii kumfurahisha mtu - Rev Lucy Natasha

Natasha alisema chumba hicho kimoja kilikuwa kila kitu kutoka malazi, jikoni na sebule.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 May 2023 - 12:21

Muhtasari


  • • "Ninataka tu kubadilisha hadithi na kupigana vita ambavyo wazazi wetu hawakuwahi kushinda,” Natasha aliandika.
Lucy Natasha akionesha maisha yake ya zamani na ya sasa.

Mchungaji mkuu wa kanisa la Oracle, Lucy Natasha amewachukua mashabiki na waumini wake katika safari ya maisha yake kwa kuwaonesha picha ya zamani akiwa mtoto.

Natasha alisimulia jinsi maisha yao yalikuwa magumu ambapo walikuwa wanarundikana kwenye chumba kimoja.

Natasha alisema wakati watu wanamuona akijibidiisha sasa hawafai kumcheka kwani anafanya hivyo sit u kuwafurahisha walimwengu bali ni kwa sababu analenga kuibadilisha na kuandika upya historia ya maisha katika amilia yake.

“Tunatoka kwa familia duni, nyumba za zamani na miji midogo yenye hadithi za kusikitisha. Hatufanyi bidii ili kuvutia au kuwa katika shindano lolote na mtu yeyote. Tunataka tu kubadilisha hadithi na kupigana vita ambavyo wazazi wetu hawakuwahi kushinda,” Natasha aliandika.

Natasha alitumia simulizi hilo kutamka Baraka kwa waumini na mashabiki wake mtandaoni akiwata kutokufa moyo kwani siku moja tu nyota yao itaangaza, akisema kuwa yeye ameona wakiinuka kutoka chumba kimoja ambacho ndicho kilikuwa kila kitu kutoka sebule, jiko na hadi kulala.

“Maombi Yangu Kwa Mtu Leo, Mungu akusaidie uweze kuwapa watoto wako zaidi ya ulivyokuwa unakua! Historia yako haibainishi Hatima yako. Chumba hiki Kimoja kilikuwa chumba cha kulala, sebule, jiko.” Natasha alitamka Imani na matumaini.

Natasha aliolewa na Nabii Carmel kutoka India na mwaka jana wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, mpenziwe alimtunuku kipande cha shamba miongoni mwa zawadi zingine.

Natasha ni mmoja wa wachungaji maarufu humu nchini haswa kwenye mitandao ya kijamii kwa jinsi wanavyojibeba katika mavazi na mahubiri pia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved