Mwanamke mmoja ameelekea mahakamani kutaka talaka kutoka kwa mumewe lakini amekumbwa na kizingiti kimoja tu.
Kwa mujibu wa taarifa, mume wa mwanamke huyo yuko tayari kumtolea talaka yake lakini kwa sharti moja – kumtafutia mke mwingine kwanza wa kuziba pengo atakaloliacha.
Aidha, mfanyabiashara wa Nigeria, Yahaya Mohammed anamtaka Hauwau Hamza amlipe sh31,186 - gharama ya mahari aliyolipa familia yake na matumizi ya nguo zake.
“Ikiwa anataka talaka, lazima anitafutie mke mwingine. Nataka mke wangu anilipe pesa zote nilizomtumia kwenye harusi yetu.”
"Nililipa ₦ 60,000 kama mahari ili kuoa mke wangu na nilitumia ₦ 100,000 kwa nguo zake, nasisitiza anilipe jumla ya pesa zote," Shirika la Habari la Nigeria linamnukuu Yahaya Mohammed akiiambia Mahakama ya Juu ya Kubwa, FCT.
Mohammed na Hamza walifunga ndoa kwa mujibu wa sheria za Kiislamu mwaka wa 2020 lakini bado hawana watoto pamoja.
Hamza alienda kortini na ombi la kutaka ndoa yake na Mohammed ivunjwe, akitaja msingi wa ukosefu wa matunzo na heshima.
Akijibu madai ya mumewe kwamba amtafutie mke mwingine kabla ya kumpa talaka, Hamza aliiambia mahakama inayoongozwa na Mohammed Wakili kwamba hangekuwa na tatizo lolote kutimiza matakwa yake lakini si ya Kiislamu.
Aliongeza kuwa Mohammed alilipa ₦ 60,000 tu kwa mahari yake na si ₦160,000 kama alivyodai.
"Sina ₦ 160,000 za kumpa, ikiwa tu anaweza kunilipa kwa kuridhika, niliyompa wakati wa ndoa na upishi ambao nimefanya kwa miaka mingi," Hamza aliiambia mahakama.
Jaji, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, alisema hakuna sheria ya Kiislamu inayomlazimisha Hamza kumtafutia Mahamed mke mwingine kabla ya kupewa talaka. Aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 17.