Mtayarishaji wa maudhui na mchekeshaji wa Kenya Dem Wa Facebook amesimulia kwa hisia jinsi babake alivyojitolea sana ili kumlipia karo ya shule, ambayo ilikuwa ikisubiriwa.
Dem Wa Facebook, kupitia chaneli yake ya YouTube, aliamua kuwafahamisha mashabiki wake jinsi baba yake alivyofanya kila awezalo kuona kwamba anapata elimu bora.
“Mimi nilijisomesha kwanzia form one nikicheza mpira, nilikua mchezaji wa mpira, halafu nikafika form three waka transfer principal tukaambiwa tulipe school fees kwanzia form one na school fees ilikua over 150."
"Imagine nikakua na stress, mimi kufika nyumbani nimefukuzwa school fees nikapata baba yangu ameuza shamba kwa sababu ya school fees yangu."
"Hii kitu inaniuma mpaka naambia Dad nataka kurudisha hii shamba sababu kwa my dad hajawahi uza shamba na hivyo juu ya school fees yangu."
Hiyo shamba ya jirani nitarudisha kwa jina la Mungu.” Dem Wa Facebook alifichua.
Ni katika chapisho hili ambapo Dem Wa Facebook aliapa kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha anarudisha shamba ambalo babake aliuza ili apate pesa za kulipia ada.
Dem Wa Facebook hivi majuzi aliweka video ya nyumba ambayo bado anaendelea kuwajegwa wazazi wake.
Dem Wa Facebook alieleza kwamba alichagua kuwajengea wazazi wake nyumba hiyo si kwa sababu ya upendo wake kwao tu bali kwa sababu yeye ndiye mlezi na anapaswa kuwa mfano mzuri kwa wengine kufuata.
“Hii nyumba nimejenga 3 months mahali tumefika ni process ya kueka mabati….na my wish ni by December nataka ikuwe ready tufungue hii Nyumba….mimi ndio breadwinner kwetu na lazima nitengeneze Nyumbani.” Dem Wa Facebook alisema.