logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Ipo siku nataka kuwa kama wewe" Wema Sepetu ampongeza mwanadada aliyeweka bango la mumewe

Wema ametoa maoni yake kuhusu bango la mahaba lililowekwa na mwanadada

image

Burudani14 February 2022 - 11:40

Muhtasari


  • •Muigizaji wa Filamu za Bongo Wema Sepetu ametoa maoni yake kuhusu bango lililowekwa na mwanadada moja  akisherekea mume wake siku ya wapendanao.
Wema Sepetu

Muigizaji wa Filamu za Bongo Wema Sepetu ametoa maoni yake kuhusu bango lililowekwa na mwanadada moja  akisherehekea mume wake siku ya wapendanao.

Wema amepenndezwa sana na video hiyo ambayo imewavutia zaidi wanamitandao huku akisifia mwanadada aliyeweka bango hilo kudhihirisha mapenzi yake kwa mumewe.

Haya yametokea baada ya video iliyokuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mwanadada aliyeweka kipenzi chake cha roho kwenye bango kubwa na kuliweka kando ya barabara ili dunia inaposherehekea Valentine's.

Hisia mbalimbali zilitolewa kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakisifia mapenzi ya mwanadada  huyu kwa mumewe.

Wema Sepetu hakusazwa nyuma huku akizamia kwenye ukurusa wake wa Instagram kupakia video hiyo  na kuwatakia wapenzi husika ndoa yenye furaha.

“Naomba nimalizie na hii apa, Na mimi ipo siku nataka kuwa kama wewe. Hii ndio njia nzuri kuonyesha kweli unapenda mtu… wenzangu na mimi naoba tutulie,kama hujamuweka kwa bango basi sio valentine wako.. Allah abariki penzi lenu,” alisema Wema

Vilevile, video hiyo  ilionekana kama kumrejesha nyuma wakati mapenzi baina ya Diamond  na Wema yalikuwa ya kupigiwa mfano


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved