logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sakata la Samidoh na Nyamu lageuka baraka kwa Edday Nderitu, aramba dili la ubalozi!

Mama mdogo amevumilia wakati mgumu ambao ungevunja wake wengi, lakini anafanya hivyo kwa heshima.

image
na Davis Ojiambo

Burudani26 April 2023 - 12:41

Muhtasari


  • • Mama mdogo amevumilia wakati mgumu ambao ungevunja wake wengi, lakini anafanya hivyo kwa heshima.
Edday Nderitu apata kazi ya ubalozi.

 Mke wa kwanza wa msanii wa Mugithi na afisa wa Polisi Samwel Muchoki almaarufu Samidoh, Edday Nderitu ni mama mwenye furaha baada ya kutumia fursa ya umaarufu ambao ameupata mitandaoni kwa miaka 3 iliyopita kujipatia dili la ubalozi wa mauzo katika kampuni moja.

Nderi alifichua habari hizo njema Jumanne jioni kupitia kurasa zake mitandaoni na kumshukuru Mungu kwa kumpa fursa kama hiyo huku akianza kuchapa kazi mara hiyo hiyo kwa kuwapendekezea mashabiki wake kuungana naye katika kujaribu biashara hiyo mpya ya mashamba.

“Nimefurahiya sana kuanza ukurasa huu mpya na The Mimshack Homes, Asante kwa Wakurugenzi kwa kuamini chapa yangu. Siwezi kusubiri kushiriki bidhaa zote za ajabu za uwekezaji wa ardhi na nyumba wanazotoa,” Nderitu alisema.

Edday Nderitu bila shaka amekuwa na mwaka wa changamoto huku akitazama picha za mumewe na mpango wake wa kando zikiendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Mama mdogo amevumilia wakati mgumu ambao ungevunja wake wengi, lakini anafanya hivyo kwa heshima.

Safari yake hatimaye ina mwisho mwema kwani kupitia umaarufu ambao amekuwa akipata japo kwa kutajwa katika matukio hasi ya mumewe Samidoh na seneta Nyamu, hatimaye umemletea dili lake la kwanza kabisa kama balozi wa mauzo.

Siku moja kabla ya kuramba dili hilo, Nderitu alidokeza kuwa anaweka Imani yake kubwa kwa Mungu kwani mlango mmoja unapofungwa, yeye humfungulia mja wake milango Zaidi.

“Wakati mlango mmoja wa furaha unafungwa, mwingine unafunguliwa, lakini mara nyingi tunatazama kwa muda mrefu kwenye mlango uliofungwa hata hatuoni ule ambao umefunguliwa kwa ajili yetu,” Nderitu alisema.

Nderitu amekuwa akipitia wakati mgumu katika kile ambacho anaonekana ni kuchoka na maisha ya ndoa na mumewe Samidoh ambaye ni wazi ameshindwa kukaa mbali na Karen Nyamu ambaye tayari wamezaa naye watoto wawili.

Nderitu aliweka bayana kwamba hayuko tayari kuwalea watoto wake katika ndoa ya wake wengi, haswa mke mwenza akiwa ni mtu asiye na stara wala chembe cha heshima.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved