Kampuni ya kuuza nyama KMC imewalipa wakulima shilingi milioni 259 ambazo walikuwa wanalidai baada ya shughuli zake kutwaliwa na Jeshi mwezi septemba mwaka huu .
Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi amesema hatua ya KDF kuchukua oparesheni za KMC imezidisha kiwango cha mifugo wanaoletwa kwa kampuni hiyo kwa asilimia 30
" Kupitia uhamisho wa shiika hilo hadi kwa wizara y Ulinzi tumefaulu kuwalipa wakulima deni lao la shilingi milioni 250’ .
Shilingi nyingine 150 zimetengwa kukamilisha madeni mengine na kwa wafanyibiashara wanaoipa hduma na bidhaa kampuni hiyo mwaka huu wa kifedha .
Matiangi ambaye anasimamia kamati ya baraza la mawaziri inayosimamia miradi ya maendeleo ya serikali ametetea hatua ya kuihamisha kampuni ya KMC kwa wizara ya Ulinzi akisema kuna uhusiano mkubwa kati ya KDF na KMC ili pia kuyalinda laslahi ya wakulima .
" Kama mteja wake mkubwa ,Jeshi lilikuwa na kikubwa cha kujinufaisha kwa kuchukua usimamizi wa oparesheni za KMC ‘ Matiang’I amesema