Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua na mke wake Pastor Dorcas wamkevunja kimya chao saa chache baada ya Kithure Kindiki kuapishwa kama naibu rais mpya.
Wanandoa hao walichukua kwenye kurasa zao kupitia mtandao wa Facebook na kuchapisha picha ya pamoja wakiwa na wanao nyumbani kwao kijijini huko Mathira, kaunti ya Nyeri.
Kwa upande wake, Gachagua katyika picha hiyo ambahyo walikuwa wameketi kwenye bustani mbele ya nyumba yake na wanawe na mkewe, alimshukuru Mungu kwa Baraka ya familia.
Gachagua alifichua kwamba upepo mwanana wa nyumbani kwake ni wa kumpa fahari kubwackatika maisha kuliko mihangaiko yote ya kisiasa.
“Nyumbani kutamu! Namshukuru Mungu kwa zawadi ya familia yangu. Harufu ya nyasi safi, sauti za ndege wanaolia ndivyo familia yenye furaha inahitaji. Nitabaki kumshukuru Mungu milele, kwa kunipa familia yenye upendo na utegemezo. Tunafurahi kuwa nyumbani, ambapo nilizaliwa na kukulia! Siwezi kungoja asubuhi ili nitembee katika Msitu wa Hombe, kufurahia mandhari nzuri ya Mlima Kenya huku nikimshukuru Mungu kwa fadhili zake,” Gachagua aliandika.
Kwa upande wa pili, Pastor Dorcus alimshukuru Mungu kwa uhai na utulivu wa nafsi licha ya kuwepo kwa dhoruba kali katika maisha ya kisiasa ya familia yaqo katika siku za hivi karibuni.
“Ni rahisi kuangalia changamoto na mazingira yanayokuzunguka na kusahau kanuni kuu ya mwamini. Leo, mimi na familia yangu tunachagua kutoa sala ya shukrani, tukielewa kwamba, Mungu anabaki kuwa mwenye enzi, iwe anatuokoa na moto au la, Danieli 3:16-18. Tunamshukuru Mungu kwa uaminifu wake wa ajabu. Tunamwita, Ebenezeri, kwa umbali huu tunamsherehekea. Tumeona rehema zake na kupata wema wake. Utukufu na heshima ziwe kwa jina lake Takatifu,’ mchungaji alisema.
Kauli zao zilijiri saa chache baada ya Kindiki kula kiapo kama naibu rais wa 3 chini ya katiba mpya ya 2010.
Kindiki aliapishwa kufuatia kubanduliwa ofisini kwa Gachagua na bunge lacseneti wiki mbili zilizopita.
Gachagua alikuwa ameshtakiwa kwa jumla ya hoja 11 ambazo ziliwasilishwa vna mbunge wa Kibwezi Magharibi, Mwengi Mutuse.