logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo Jumamosi

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na   Nairobi, West Pokot na Nyeri.

image
na SAMUEL MAINA

Habari25 May 2024 - 05:57

Muhtasari


  • •KPLC imetangaza baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na   Nairobi, West Pokot na Nyeri.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumamosi, Mei 25.

Katika taarifa ya siku ya Ijumaa jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na   Nairobi, West Pokot na Nyeri.

Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za mtaa wa Westlands zikiwemo ABC Place, Manyani, Delloite, Westend Tower, sehemu za Waiyaki Way na viunga vyake zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za  eneo la Kapenguria katika kaunti ya West Pokot zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za mji wa Karatina katika kaunti ya Nyeri pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved