KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea Alhamisi

KPLC)imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Mei 2.

Muhtasari

•KPLC ilisema baadhi ya maeneo ya kaunti 5 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Mei 2.

Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na  Nairobi, Samburu, Nyeri, Murang'a na Kilifi.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu kadhaa za mtaa wa Peponi zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Mji mzima wa Maralal na eneo la Posta katika kaunti ya Samburu kutakuwa bila umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti za Murang'a na Nyeri, baadhi ya sehemu za maeneo ya Kiriani na Kamune zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Shamba la Kilifi katika kaunti ya Kilifi pia litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.