logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watumiaji wapya wa X watalazimika kulipa Sh150 kwa mwaka ili tu kuchapisha kwenye jukwaa

Ada hii ni kwa akaunti mpya ambazo hajijathibitishwa wala si akaunti zilizopo tayari.

image
na Davis Ojiambo

Habari18 October 2023 - 08:55

Muhtasari


  • •Mnamo Oktoba 5, Bloomberg iliripoti kuwa X ilikuwa inapanga kujaribu viwango vitatu vya huduma ya kulipia kwa watumiaji kulingana na idadi ya matangazo yaliyoonyeshwa.
  • • X hakubainisha ikiwa sera hiyo hatimaye itatanuliwa kwa watumizi wa X katika nchi zingine.

X ya Elon Musk, ambayo awali ilijulikana kama Twitter, imeanza kutoza watumiaji wapya nchini New Zealand na Ufilipino ada ya $1, sawa na shilingi 150 za Kenya kila mwaka ili kutumia jukwaa hilo.

Kwa mujibu wa Business Insider Africa, Sera hiyo, ambayo inaanza leo, iliripotiwa kwa mara ya kwanza na Kylie Robinson wa Fortune siku ya Jumanne.

Ilithibitishwa haraka na jukwaa lenyewe iliposema kwamba ilikuwa ikifanya majaribio mpango wake mpya wa "Not A Bot" katika nchi hizo mbili. X hakubainisha ikiwa sera hiyo hatimaye itatanuliwa kwa watumizi wa X katika nchi zingine.

Kama sehemu ya jaribio, "akaunti mpya, ambazo hazijathibitishwa" zitalazimika kulipa ada ya usajili ya kila mwaka ya $1 "ili kuweza kuchapisha na kuretweet machapisho mengine." Watumiaji waliopo hawataathiriwa na jaribio, jukwaa hilo lilinukuliwa na Business Insider Africa.

Jukwaa liliongeza kuwa sera mpya haikuwa "kiendeshaji faida" na badala yake ilikusudiwa kupunguza ushawishi wa roboti.

Musk na kampuni yake wametafakari kwa muda mrefu kufanya mabadiliko kwenye mipango ya malipo ya jukwaa.

Mwezi uliopita, Musk alimwambia waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, wakati wa mtiririko wa moja kwa moja kwamba X inaweza kuanzisha paywall ya malipo kwa watumiaji wake wote.

"Kwa kweli tutakuja na bei ya kiwango cha chini. Tunataka iwe kiasi kidogo tu cha pesa," bilionea alisema wakati huo. "Ni majadiliano marefu, lakini kwa hakika huu ndio utetezi pekee dhidi ya majeshi ya roboti."

Mnamo Oktoba 5, Bloomberg iliripoti kuwa X ilikuwa inapanga kujaribu viwango vitatu vya huduma ya kulipia kwa watumiaji kulingana na idadi ya matangazo yaliyoonyeshwa.

Musk amefanya mabadiliko mengi kwenye jukwaa tangu alipoipata Oktoba 2022.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved