logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu watano wafariki baada ya kubugia pombe haramu Bungoma

Wawili wanaendelea kupokea matibabu

image
na SAMUEL MAINA

Habari24 March 2022 - 03:30

Muhtasari


  • •Waathiriwa wanaripotiwa kulalamika kuumwa na tumbo na uchovu mwingi mwilini baada ya kunywa pombe hiyo
Chang'aa

Watu watano walifariki na wengine 10 kulazwa hospitalini baada ya kubugia pombe haramu katika kijiji cha Canaan, eneo la Kimilili.

Walionusurika kwenye tukio hilo la Jumatano asubuhi walikimbizwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Kimilili ambako walihudumiwa na kuondoka. Wawili wanaendelea kupokea matibabu.

Miongoni mwa waliolazwa ni pamoja na mwanamke aliyetengeneza kileo hicho kinachoaminika kuwa chang'aa.

Waathiriwa wanaripotiwa kulalamika kuhusu kuumwa na tumbo na uchovu mwingi mwilini baada ya kunywa pombe hiyo. Wanne walifariki papo hapo huku mwingine akiripotiwa kufariki baadae.

Inashukiwa kuwa pombe hiyo iliyopigwa marufuku nchini ambayo wahasiriwa walikunywa ilikuwa na kemikali zenye sumu.

Wanakijiji waliomba hospitali kuchunguza sumu ambayo ilikuwa ndani ya kileo hicho.

Mjumbe wa wadi ya Kibingei Aggrey Mulongo aliagiza serikali ya kaunti kuunda sera za kudhibiti unywaji ya chang'aa na busaa.

Tukio hilo linakuja takriban wiki moja tu baada ya mtu mmoja kufariki na wengine watatu kulazwa hospitalini baada ya kunywa pombe haramu katika kaunti ya Uasin Gishu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved