logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume amuua babake, mama wa kambo na kujiwasilisha kwa polisi akiwa na silaha ya mauaji, Meru

Kando ya mwili wa babake kulikuwa na mwili wa mama wa kambo Eunice Kangai, 38.

image
na Davis Ojiambo

Habari15 March 2024 - 05:48

Muhtasari


  • • Mwili wa Kirimi alikuwa na alama kubwa za kukatwa kwenye mkono wa kulia, upande wa kulia wa kichwa, kiganja cha kushoto na bega la kushoto yote yakiwa yamesababishwa na kifaa chenye ncha kali.
Panga. Silaha ya muuaji inasemekana alitumia kumuua babake na mamake wa kambo huko Meru mnamo Machi 14, 2024. Picha: MAKTABA

Mwanamume mmoja aliwachinja babake na mamake wa kambo katika kisa cha kusikitisha kabla ya kujisalimisha kwa polisi na akiwa silaha ya mauaji katika eneo la Kiirua, Kaunti ya Meru.

Mkazi mmoja alikuwa amewaarifu polisi katika kituo cha polisi cha Kiirua mnamo Alhamisi, Machi 14 jioni kuripoti kuwa mwanamume mmoja alikuwa amewaua watu wawili katika eneo la Kibirichia katika Kaunti Ndogo ya Buuri Mashariki kabla ya mshukiwa kuwasili katika kituo cha polisi akiwa na silaha ya muuaji iliyokuwa na madoa ya damu.

Alikamatwa na kufungiwa kwenye seli. Mshukiwa ni mwanaume mwenye umri wa miaka 35.

Polisi baadaye walitembelea eneo la tukio na kupata mwili wa babake mshukiwa aliyetambulika kama Julius Kirimi, 67, ukiwa umetapakaa damu.

Kando ya mwili wake kulikuwa na mwili wa mmoja wa wake zake aliyetambulika kama Eunice Kangai, 38.

Kirimi alikuwa na alama kubwa za kukatwa kwenye mkono wa kulia, upande wa kulia wa kichwa, kiganja cha kushoto na bega la kushoto yote yakiwa yamesababishwa na kifaa chenye ncha kali.

Mwili wa Kangai ulikuwa na alama za kukatwa katika mkono wa kushoto wa juu, shingo, kichwa na sikio la kulia.

Polisi walisema walikuwa wameambiwa familia hiyo ilikuwa na ugomvi kuhusu kipande cha ardhi, jambo ambalo wanashuku kuwa lilisababisha shambulio hilo baya.

Maafisa hao wa usalama walihamisha miili hiyo hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti wakisubiri uchunguzi wa maiti na uchunguzi mwingine.

Polisi walisema kuwa silaha hiyo ya mauaji-panga- ilihifadhiwa kama kielelezo huku uchunguzi ukiendelea.

Polisi walisema kwamba mauaji ya aina hiyo yanazidi kuongezeka katika kaunti hiyo huku migogoro ya ardhi na mingine ya ndani ikiwa ndio sababu kuu za uhasama.

Polisi wanasema baadhi ya kesi za mauaji zinaendelea mahakamani huku nyingine zikiwa chini ya uchunguzi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved