In Summary

•Mchekeshaji Othuo Othuol, alisaidiwa na daniel Ndambuki almaarufu Churchill

•Zeddy apongeza usimamizi wa chuechill, kwa kazi yao nzuri

•Churchill alisimama na Othuo wakati wa ugonjwa wake, na alienda kumtembelea siku mbili kabla ya kifo chake

Zeddy Zainabu 16508539_686417551538056_4275234156423186793_n
Image: Hisani

Siku chache baada ya ifo chake mcheshi Othuol Othuol kutokea mchekeshaji Zeddy Zainabu amejitokeza na kutetea bosi wake Daniel Ndambuki almaarufu Churchill.

Hii ni baada ya Churchill kupokea ukosoaji mkubwa kutoka kwa wakenya kuwa hajakuwa akimsaidia mwendazake.

Haya yanajiri baada ya awali kabla ya kifo chake Othuol kusema kuwa churchill amekuwa akimsaidia sana katika maisha yake na kuwa alilipa gharama ya hospitali aliplazwa wakati wa kwanza.

 

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Zeddy aliandika ujumbe mrefu unaosoma,

"Nina huzuni mwingi nikiandika ujumbe huu kwanza ni kwa kumpoteza ndugu yetu Othuol,pili nimeona jumbe watu wanatuma kuhusiana na kifo chake.kuna mambo mengi najua lakini sitataja yotelakini machache nitayasema.last tiimeniliongelea churchill management na nikawakashifu but leo niko hapa kurudisha shukrani kwa@Kariscomedian na @Eddiebutita kwa kumpeleka Othuol Hossy na churchill kwa kusimama na othuol wakati alikuwa mgonjwa

Mara ya kwanza Otuol kungojeka bill ya hospitali ililipwa na churchill,Othuol amelazwa hossy most times na churchill akacome through." Aliandika Zeddy.

Pia Zeddy alisema kuwa Churchill alienda kumtembela Othuol siku mbili kabla ya kifo chake,

"2 days before Ohuol atuache churchill alienda kenyatta pekeyake kumuona na reason naandika hivi ni juu alituambia kama wasanii tukamuone

Alituma ujumbe kwa kikundi cha wasanii hapo nakupongeza kwa kuonyesha utu na kutukumbusha vile tunafaa kusaidiana kama wasanii pia nashukuru @mbili na @ sandra-dacha wa Auntie boss kwa kuwa mstaari wa mbele kutembelea ndugu yetu na hukuchokankuchangishia Othuol."

Zeddy alisema kuwa kitu ambacho watu na wakenya wanapswa kufahamu ni kuwa Churchill alisimama na Othuol kabla na wakati wa ugonjwa wake.

 
 

"So kitu nataka watu wajue ni kuwa churchill alisimama na othuol kabla na wakati wa ugonjwa wake yeye si mtu wa kujionyesha na angekuwa hiyo type angetuonyesha kwa sasa sitaki tuseme mengi lakinii mnuruhusu nimuomboleze kaka yangu,safiri salama Benmorris ouma."

 

View Comments