In Summary
  • Nimeacha kuwa mtu mzuri akothee asema
  • Jambo lolote nzuri au mbaya utakalo ambiwa na mtu kunihusu muamini
scsc

Msanii Akothee kwa muda amekuwa akiwakashifu watu kwa maana baada ya kuwasaidia wanamgeuka na kusema kuwa yeye ndiye mbaya.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram hii leo amesema kuwa ameacha kuwa mzuri kwa watu na kuwa kama binadamu yeyote yule.

"Nimeacha kuwa mzuri na kuwa kama binadamu, watu wengi wanataka tuzungumze ana kwa ana wakifikiri mimi ni mjinga kuja kujifurahisha

 

Naweza fanywa mjinga mara moja na kuuizwa roho na mtu mmoja mara ya pili kwa kweli ni kwa ajili ya kosa langu na ninapaswa kujipa mashaka yangu mwenyewe." Aliandika Akothee.

Huku akizungumzia mambo ambayo wengi husema kumhusu yawe mema au mabaya alisema kuwa watu wanapaswa kuamini  kwa maana hilo ndilo walienda kumfahamu nalo na wakarudi nalo.

"Kwa hivyo jambo lolote la hasi ambalo utalisikia kunihusu kutoka kwa watu ambao walipata fursa ya kunijua tafadhali jambo nzuri au la hasi waamini

Hilo ndilo walikuja nalo na wakalipata jinala ngu ni Esther Akoth Kokeyo ata wakinipa jina la Ivan waamini na kama huwezi amini call police."

Akothee pia alisema kama masengenyo ni  mali ya kupeleka benki na kupata mkopo wanaweza fanya hivyo wala wasiharibu mali yao kwa kukalia.

View Comments